Na Karoli Vinsent
Miezi michache kupita tangu Rais Jakaya
kikwete kupangua Baraza lake la Mawaziri,hivi leo Waziri wa Maliasili na
Utalii,Lazaro Nyalandu ameanza kumliza Rais kiwete baada ya kubuni mradi
unaoendana na mradi wa Buzwagi.
Mradi wa Buzwagi ambao uliwezesha serikali
ya Jakaya kiwete kutoa Mgodi waDhahabu wa Shinyanga kwa bei ya Kutupwa kwa
wawekezaji wa Kigeni.Nyalandu amemliza Rais Kikwete ambaye alitaka kuwepo
tahadhari na upembuzi wa Kina katika utelekezaji kazi.
Kipindi alipokuwa Waziri wa Nisharti na
Madini,Naziri Karamagi alifunga safari na kwenda hadi wingereza kukutana
na wawekezaji na kusaini mikataba kwenye Haoteli za uingereza badala ya
kukutana kwenye barozi za Tanzania nchini uingereza.
Kile kinachoonekana Hivi sasa nae waziri
wa Nyalandu anafuata nyayo za Waziri wa Karamagi,hivi leo Nyalandu amefunga
safari kwenda Afrika kusini kwenda kukutana na wakurugenzi wa kampuni inayotaka
kukabidhiwa Hifadhi za wanyama kwa ajili ya kuwinda na kufanya utalii wa picha.
Kwa
Mujibu wa Vyanzo vya kuaminika ambazo Mwandishi wa Mtandao huu ameziona zinasema
waziri nyalandu katika safari hiyo amewafuata kampuni ya African Parks
Network(APN) ambao wanashikiza kupewa kuruhusiwa kupewa Hifadhi mbalimbali.
Kampuni
hiyo ya APN ni Uholanzi ambapo makao makuu yake nchini Afrika kusini,kampuni
hiyo ambayo imewahi kuendesha Hifadhi hapa Afrika ikwemo Ethopia na
kuleta matatizo makubwa ikwemo kwa Wananchi na kupelekea nchi hiyo kuvunja
mikataba ya Kampuni hiyo.
Kwa Mujibu
wa Chanzo hicho kinasema Kampuni hiyo APN inampango wa kupewa Hifadhi ya
Katavi,huku Waziri Nyalandu akishinikiza kumpuni hiyo Hifadhi pasipo kuangalia
athari za kampuni hiyo kwa Taifa na Wananchi kwa Ujumla.
Wadau
mbalimbali wa waliozungumza na Mwandishi wa Mtandao huu wanasema kuna haja
ya Taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU kuanza Kumchunguza Waziri
Nyarandu kutokana na Haraka aliyekuwa nayo ya kwenda kuifuata kampuni hiyo nchi
Nyingine je huku kulikuwa hakuna maslai binafsi kati ya Nyalandu na Kampuni
hiyo?
Kwa
upande wake waziri Kivuli wa Maliasiri na Utalii Mchungaji Piter Msigwa
alipotafutwa na Mwandishi wa Mtandao huu alisema yeye amelisikia suala hilo
kwenye Baadhi vyombo vya Habari na yeye analikamilisha sakata hilo na
atalitolea Taharifa baada ya kupata taarifa za kutosha.
Msigwa
ambaye ni mbunge wa Iringa Mjini Kupitia Chama cha Demokrasi Chadema alizidi
kusema yeye anamngoje waziri Nyalandu atakaporudi ndio kwa upande wao waliweke
wazi suala hilo.
No comments:
Post a Comment