Friday, April 25, 2014

NAIBU WAZIRI WA KAZI DK MAKONGORO MAHANGA AFUNGUA KONGAMANO LA AFYA NA USALAMA KATIKA MATUMIZI YA KEMIKALI SEHEMU ZA KAZI NDOGO


 Washiriki wakijiandikisha nje ya ukumbi kabla ya kuanza kwa kongamano la afya na usalama katika matumizi ya kemikali sehemu za kazi
 Zoezi la uandikishaji na uhakiki wa majina ya washiriki wa kongamano ukiendelea
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa kazi Mhe Dk Makongoro Mahanga akiingia ukumbini
 Wajasiriliamali wakiwa wamesimama kumpokea Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa kazi Dk Makongoro Mahanga
 Dk Akwilina Kayumba akitoa neno la kumkaribisha Naibu waziri wa kazi ndani ya ukumbi wa ILO jijini Dar es salaam
 Meza kuu ya wageni waalikwa kutoka kushoto ni Joshua Matiko Director Training wa Osha,Anayeongea ni Dk Akwilina Kayumba mkurugenzi mkuu kutoka Osha,Wa tatu kushoto ni Naibuwaziri wa kazi Dk Makongoro Mahanga na Wanne kutoka kushoto ni Frank Muchiri kutoka ILO.
 Meza kuu wakisikiliza kwa umakini utambulisho wa washiriki wa kongamano hilo
 NaibuWaziri wa kazi Dk Makongoro Mahanga akisikiliza utambulisho kutoka kwa washiriki wa kongamano
 Washiriki mbalimbali wa kongamano la Afya na usalama katika matumizi ya kemikali sehemu za kazi ndogo wakifuatilia kwa utambulisho kutoka kwa washiriki wenzao.
 Washiriki wa kongamano la afya na usalama katika matumizi ya kemikali wakifuatilia kwa ukaribu maelezo na ufafanuzi wa Mada kuu ya kongamano
 Bi Julieth Mushi ambaye ni mjasiriamali wa kutengeneza mikate akijitambulisha kwa washiriki wenzie wa kongamano la Afya na usalama katika matumizi ya kemikali katika ukumbi wa ILO jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Kazi Dk Makongoro Mahanga akisoma hotuba ndani ya ukumbi wa ILO tayari kwa ufunguzi wa kongamano la usalama katika matumizi ya kemikali.
 Kutoka kushoto ni Mwakilishi kutoka ILO Frank Muchiri na Dk M.Kapalata kutoka TUCTA
  Dk M.Kapalata kutoka TUCTA akitoa mada kuhusiana na afya na usalama katika matumizi ya kemikali

Washiriki wa kongamano wakiendelea kusikiliza kwa umakini mafunzo na mada kuhusu matumizi ya kemikali

Picha ya pamoja ya washiriki wa kongamano na Mgeni Rasmi Dk Makongoro Mahanga
 Dk Makongoro Mahanga ambaye ni Naibu waziri wa kazi akiagana na washiriki wa kongamano la afya na usalama katika matumizi ya kemikali nje ya ukumbi wa ILO.
Naibu waziri wa kazi na ajira Dk Makongoro Mahanga amefungua kongamano  la afya na usalama katika matumizi ya kemikali sehemu  za kazi ndogo. Akitoa hotuba yake Naibu waziri huyo amesema inatakiwa elimu na maelekezo mazuri yatolewe kwa wajasiriamali wadogo na wakubwa kuhusu matumizi ya kemikali na usalama wa matumizi wa kemikali hizo.


Naibu waziri wa kazi na ajira aliongeza kwa kusema ripoti ya shirika la kazi duniani (ILO) ya mwaka 2004 inaonyesha kwamba,Duniani kote magonjwa yanayotokana na kemikali nii kwa kupitia njia ya hewa,maji,kazi nauvutaji wa moja kwa moja.Mnamo mwaka 2004 ilionekana kulikuwa na Vifo milioni 4.8 ambayo ni sawa na asilimia 8.3% na vilema milioni 86 sawa na asilimia 5.7% ambavyo vilisababishwa na matuimizi yasiyo sahihi ya kemikali.
 

No comments: