Mwenyekiti wa jukwaa la katiba tanzania DEUS KIBAMBA |
Na
Exaud mtei
Jukwaa
la katiba Tanzania JUKATA limejitolea kuratibu maridhiano miongoni mwa makundi ya kisiasa asasi za kiraia asasi za wananchi na taasisi
zote za muhimu zilizoguswa na migogoro inayoendelea katika bunge maalum la
katiba tanzania
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za jukwaa la katiba sinza jijini dare s
salam mwenyekiti wa jukwaa la katiba bw DEUS KIBAMBA juu ya tathimini walizozifanya katika bunge
hilo wameamua kujitolea kufanya maridhiano hayo kwa kuwashirikisha viongozi
maarufu afrika ya mashariki akiwemo
mheshimiwa jaji mkuu mstaafu wa Tanzania BARNABAS SAMATTA ambaye atakuwa mkuu
wa jopo hilo la usuluhisho nandugu PATRICE LUMUMBA kutoka Kenya ambaye atakuwa msaidiz
Aidha jukwaa hilo limeonyesha
masikitiko yake kwa kile walichookiita ni uvunjifu wa kanuni mara baada ya
wabunge zaidi ya mia mbili kutoka nje lakini wabunge waliobakia kuendelea
kurekebisha kanuni za bunge hilo jambo ambalo wamesema kuwa haikustaili kwani
wana uwezo wa kujitungia sheria.
KIBAMBA
amesema kuwa kutokana na mwenendo wa bunge hilo hadi hapa lilipofikia wabunge
hao hawana nia ya dhati ya kulipatia taifa katiba mpya huku akitolea mfano kuwa
katiba mpya ilipangwa kuwekwa saini na Rais
siku ya tarehe 26 mwezi huu yani kesho
lakini hadi sasa hata majadiliano ya sura mbili hayajamalizika, na
kuwahakikishia watanzania kuwa hakuna katiba mpya itakayopatikana kwa mwaka
huu.
Hata hivyo mwenyekiti huyo amewataka
wajumbe wote na asasi zote zilizopo nje ya muendelezo wa bunge hilo maalumu la
katiba kuwa tayari kwa maridhiano kwa mtu au taasisi yoyote atakayekuwa tayari
kutatua migogoro yao ili kuwezesha upatikanaji wa katiba kwa taifa letu
No comments:
Post a Comment