VITENDO vya kutapanya
madaraka na kurundika vyeo kwa Makada wa chama cha Mapinduzi
CCM,kunavyofanywa na Rais jakaya Kikwete,kunazidi kuibua kelele kutoka kwa
wananchi huku wengi wao wakiishia kuumia kutokana na mambo yanayoendele hapa
nchini.
Uchunguzi uliofanywa na Mwandishi wa
Mtandao huu umebaini Mikoa ya Rukwa na Iringa.na Wilaya za kiteto,hazitakuwa na
Viongozi wa Serikali(Wakuu wa Mkoa na Wilaya) kwa kuwa takribani miezi saba
watakuwa wakishiriki vikao vya Bunge maalum la katiba,ambalo wiki chache
litafuatiwa na Bunge la bajetila serikali ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania.
Ni dhahiri kumalizika kwa bunge
hilo,itakuwa mwanzo wa kuanza kwa mkutano mrefu wa bunge la bajeti ambalo
litachukua miezi miwili.
Kwa mujibu wa Chanzo cha chetu kinasema
kwa muda wote huo,mikoa ya Iringa na Rukwa haitakuwa na viongozi wake na wakuu
katika mikoa na Wilaya,
Wilaya za Uyui,Meatu na kiteto,hazitakuwa
na Wakuu wake kwa kuwa viongozi wake watakuwa wakiishi mjini Dodoma katika
vikao vya Bunge la bajeti na la Katiba.
Sababu ya kutokuwepo katika nafasi zao
za utawala ni kutokana viongozi hao kuwa katika nafasi ya Viti maalum
ungeni,viongozi hao ni Stella Manyanya ambae ni Mkuu wa mko wa Rukwa,Christina
Ishengoma vilevile naye ni mkuu wa mkoa wa Iringa.
Kwa upande wa Wakuu wa Wilaya Ya
Kiteto Rose Kamili, Mkuu wa Wilaya ya Meatu na Lucy Mayenga mkuu wa
Wilaya Uyui.
Kuwepo kwa Viongozi hawa mjini
Dodoma,kumetoa Mwanya kwa Wafanyakazi kutoka katika Halmashauri hizo kuanza kufanya
vitendo vya kifisadi huku wananchi wakiteseka kutokana na kutokuwepo kwa
Usimamizi kutoka kwa viongozi hao.
Akizungumza,na mwandishi wa mtandao
huu,mmoja wa wafanyakazi kutoka katika Wilaya ya Meatu,ambaye amekataa
kutaja Jina lake kwenye Mtandao huu,amesema kwa sasa Huduma za kwa sasa
haziendi vizuri kutokana na Watumishi kuzembea kutokana na mkuu huyo kutokuwepo
ofisini.
“Ndugu Mwandishi katika familiya
yoyote hasipokuwepo Baba basi akuna kinachofanyika,ndio maana hata hapa
leo huduma zinakwenda taratibu,na watu wamegeuza Halmashauri hii kuwa uwanja wa
Soga tu”
“Huku watu wakija kupata huduma
hususani waalimu kusota tu,na kama viongozi hawa wangekuwepo basi huduma
zisingekuwa legelege hivi”alisema Mtoa Taarifa hiyo
Duru za kisiasa zinasema wa
kulaumiwa kwa hali hiyo ni Rais Jakaya Kikwete ambaye amekuwa akitapanya
madaraka kwa watu huku akijua mtu anaempa uongozi Teyali ni kiongozi sehemu
nyingine.
Rais Kikwete amekuwawa akiwatajirisha
watu wachache kwa kitendo chake hicho, huku wananchi wakiwa wanaumia na hali
hiyo kutokana na ufanisi wa kazi kuwa mdogo kutokana na viongozi hao kushindwa
kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja.
Huku Taifa hili likiwa na
Wasomi wengi ambao wamekuwa wakiangaika kutokana na Tatizo la ajira,huku yeye
akijinadi kuwa ni mtatuzi wa tatizo hilo.lakini la ajabu tumeshuudika katika
utawala wake amekuwa akiwapa makada wa Chama chake kazi mbili kwa wakati
mmoja,huku akisau ahadi zake.
Nikiwa na Tafakari kuhusu kuandika
makala hii kutokana na Unyama huu kwa Watanzania kwa kutapanya Madaraka
kunavyofanywa na Rais Kikwete.
Hivi,leo tumeshuudia,Rais huyu huyu
Kikwete amemteua Waziri wa Nchi Ofisi Rais,kazi maalum.Profesa Mark Mwandosya
kuwa mkuu mpya wa Chuo Kikuu cha Sayansi cha Sayansi na Teknolojia mbeya(MUST)
cha mkoani Mbeya huku akiwaacha watanzania wenye sifa ya kusimamia nafasi hiyo.
Wachambuzi wa siasa wanasema
anachokitetea rais_urundikaji madaraka mengi kwa mtu mmoja si utamaduni mzuri
hata kidogo kwa kigezo chochote kile,Nchi inao watu wenye uzoefu na waliobobea
kwenye nafasi hiyo.
Swali la kujiuliza je tutalajie nini
katika Taifa hili kwa viongozi wenye Nafasi zaidi ya moja ya uongozi,huku
nafasi hizo ni nafasi kubwa katika ufanyaji wa Kazi,hivi leo hao wakuu wa mikoa
na wa wilaya wako Dodoma je wanajua kinachoendelea kwenye mkio yao?
Je kama Rais Kikwete alikosa watu
wenye Sifa katika kuongoza nafasi hizo kulikuwa na Ulazima gan kuteua hao wakuu
wa wilaya huku akijua wananafasi zengine?na kwanini asingeaacha nafasi hizo
wazi au lengo lake lilikuwa kuwatajilisha makada wenzake kwa utajili kutokana
na mtu mmoja kuwa na kazi zaidi ya mbili.
Tafakari
No comments:
Post a Comment