mkuu wa kitengo cha fedha kutoka tigo bw ANDREW HODGSON alipokuwa anazungumza juu ya huduma hiyo mpya |
Tigo Tanzania leo imeingia katika record
nyingine baada ya kutangaza rasmi kuwa imeingia katika ushirikiano na mabenk
makubwa 17 nchini kwa ajili ya kuwapatia huduma wateja wake wa tigo pesa na
kuwapa wateja wake uwezo wa kupokea fedha kutoka katika account nyingine za
benk kwenda simu za mkononi.
Katika uzinduzi huo kampuni ya tigo
imetangaza kuwa wateja wa tigo watakuwa wana uwezo sasa wa kutoa na na kuweka
fedha kwa masaa 24 kupitia tigo pesa kutoka katika akaunti zao za mabenk 17
makubwa nchini .
Akizungumza na wanahabari leo jijini dare
s saalm mkuu wa idara ya fedha kutoka tigo ANDREW HODGSON amesema kuwa huduma
hii mpya inatarajiwa kutimiza malengo ya kampuni yao ya kuwapatia wateja wake
uhalisia wa maisha ya kidigitali kwa kuwawezesha kupata huduma za account zao
za benk kutoka sehemu yoyote walipo kupitia simu zao za mkononi
Aidha amesema kuwa kwa kutumia huduma
hii wateja watakuwa na njia salama ya haraka zaidi ya kupata fedha na kuepuka
kutembea na idadi kubwa ya fedha mkonono jambo ambalo ni hatari kwao.
Waandishi wa habari mbalimbali wakiwa wanamsiliza kwa makini mkuu wa kitengo cha fedha kutoka tigo bw ANDREW HODGSON alipokuwa anazungumza juu ya huduma hiyo mpya |
No comments:
Post a Comment