Waziri wa maendeleo ya mifugo na uvuvi dk
TITUS MLENGEYA KAMANI leo ametoa pongezi kubwa kwa kampuni ya simu za mkononi
ya tigo Tanzania kwa kuanzisha kitengo cha tigo kilimo ambacho kitawasaidia
watanzania wengi kutumia mtandao huo kujiendeleza katika maswala ya kilimo
ufugaji na uvuvi hapa nchini
Waziri huyo ameyasema hayo leo jijini dare s salaam
katika maonyesho ya kilimo yaliyofanyika katika ukumbi wa mlimani city hapa
jijini ambapo alipata nafasi ya kutembelea mabanda mbalimbali na kuona shughuli
ambazo zinafanywa na wadau mbalimbali wa kilimo
Moja kati ya mabanda Aliyotembelea waziri
huyo ni banda la kampuni ya simu za mkononi ya tigo ambalo limekuwa na kitengo
maalum cha tigo kilimo yenye lengo la
kuwasaidia wafugaji na wakulima nchini.
No comments:
Post a Comment