Timu ya Watoto
wa Mitaani ya Tanzania iliyotwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani nchini
Brazil baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 kwenye fainali imetambulishwa leo (Aprili
11 mwaka huu) katika Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma.
Baadaye
timu hiyo leo itapata chakula cha mchana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mizengo Pinda. Saa 10 jioni itatembeza kombe hilo katika maeneo
mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma katika gari za wazi.
Timu ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania iliyotwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani nchini Brazil baada ya kuifunga Burundi mabao 3-1 kwenye fainali, imetambulishwa leo (Aprili 11 mwaka huu) katika Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma. |
Jioni
imeandaliwa hafla maalumu ya chakula pamoja na burudani hapo hapo mjini Dodoma
ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk.
Fenella Mukangara.
No comments:
Post a Comment