Muongozaji mkongwe wa filamu nchini Tanzania mwenye asili ya Kenya, George Tyson amefariki Dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari wakati wakitokea kwenye hafla ya kuadhimisha miaka miwili ya kipindi cha luninga cha The Mboni Show mkoani Dodoma kufuatia gari walilokuwa wakisafiria aina ya Toyota Noah kupasuka matairi na kuangukaeneo la Gairo mkoani Morogoro majira ya saa moja jioni.
Katika gari hilo walikuwa watu 8 ila yeye pekee ndio aliyepoteza maisha na wengine kupata majiraha mwilini pamoja na dereva wa gari hilo. Kwa sasa mwili wa marehemu umehifadhiwa hapa Morogoro katika hospital ya mkoa Morogoro, baadae asubuhi mwili utaanza safari ya kurudi Dar es Salaam
Awali Tyson aliwahi kuwa mume wa muigizaji nyota wa kike wa Bongo Movie, Yvonne Cherry ‘Monalisa’ aliyeza nae mtoto mmoja wa kike anayeitwa Sonia.
Atakumbukwa kwa ucheshi, ukarimu na busara zake, Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahali pema peponi Ameen.
No comments:
Post a Comment