Na Karoli Vinsent
KATIBU
wa chama cha Mapinduzi CCM,Abdulrahman
Kinana,anatarajiwa Kugombea Urais kwenye Uchaguzi mkuu mwakani 2015.
Taarifa hizo
ambazo Mtandao huu umedokezwa,zinasema kitendo cha Katibu mkuu huyo
kuingia kwenye Kinyanganyiro hicho zinalenga Kuwanyamazisha Makada mbalimbali
ndani ya Chama hicho ambao wamekuwa wakitumia kila Njia kuhakikisha wanashika
nafasi hiyo ya Urais kwenye uchaguzi mkuu mwakani.
Makada mbalimbali ndani ya chama cha
Mapinduzi CCM ambao wamekuwa wamejitokeza Hadharani kutaka nafaisi hiyo ni ,
Edward Lowassa, Bernard Membe,Stivin Wassira, Frederick
Sumaye,William Ngereja,January Makamba,Samweli Sitta mala kadhaa wamekuwa
wakiitaji Nafasi hiyo.
Chanzo
hicho kinasema sababu kuu inayomfanya katibu mkuu huyo Wa CCM,kuingia katika
Kinyanganyilo hicho ni kutokana na Uwezo aliouonyesha ndani ya Chama na kuanza
kukubalika kwa Wananchi.
Akilizungumizia
hili Mjumbe wa Halmashauri kuu NEC ya Chama cha Mapinduzi CCM,ambaye
anatokea Mikoa ya Kusini,huku hakutaka Jina lake litajwe Kwenye
Mtandao huu anasema,kasi ya Kinana inatishia wasaka Urais.
“Sikufichi
Mwandishi kasi aliyoanza nayo katibu wetu Kinana ni kubwa sana,Maana chama
kilipoteza mvuto kwa Wananchi ila baada ya kuchagulwa Jembe hili Kinana,hari
imekuja kwenye chama chetu na Sikufichi huyu lazima awashangaze wengi mwakani
kwani anakila aina ya Sifa ya kugombania Urais”
“Na
lazima wasaka Urais, ambao wanapita kwenye makanisa na misikitini wakiomba
Huruma ya wananchi ili waonekane wasafi,wapate madalaka kiukweli huyo mzee
Kinana lazima agombanie Urais”alisema Mjumbe huyo wa Halamshauri Kuu ya NEC.
Duru zinasema Katibu mkuu huyo,kuanza
kuonyesha Dalili hizo kunazifanya zile Kambi za Wasaka Urais wa Chama hicho,kuanza
kuweweseka na kushindwa wajue wafanyaje ili waweze kuipunguza nguvu kasi ya
Kinana.
Mbio hizo za Kinana zinameibuka ikiwa ni Miezi
michache kupita baada ya Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi
(CCM),kuwafungia wasaka hao wa Urais kwa mda wa Miezi 12,kutafanya Vitendo
hivyo vya kutaka Urais.
Makada
hao ambao, waliohojiwa niWaziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya kampuni tata ya
kufua umeme ya Richmond, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli,Edward
Lowassa, wengine waliohojiwa kwa nyakati tofauti katika ukumbi
maarufu kama White House mjini Dodoma ni Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya
Tatu, Frederick Sumaye pamoja na aliyepata kuwa Waziri wa Nishati na Madini,
William Ngeleja.
Viongozi
hao walihojiwa kutokana na kile kinachoaminika ni kuanza kampeni za kusaka
urais 2015 kupitia CCM kabla ya wakati rasmi kuwadia, huku wakichezeana rafu na
matumizi makubwa ya fedha yakihusishwa.
Akizungumzia
kitendo hicho cha Katibu mkuu huyo wa Chama kikongwe kabisa Afrika ambacho kipo
Madarakani ,Msomi wa Masuala ya kisiasa kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Seiph
Yahaya,alisema kitendo hicho cha Katibu Kinana kuingia kwenye Kinyang”anyilo
alisema kinaweza kukipeleka chama hicho kwenye misuguano isiyokuwa na Lazima
kwani uwezo wake hawezi kuendana na Kasi za Siasa
“Kiukweli
ndugu mwandishi acha Nikwambie, ukweli uwezo wa Kinana haendani na kasi ya sasa
ya Taifa lilipofikia kwani Taifa linamabadiliko mengi sana hebu angalia
changamoto atakzoachiwa na Rais Kikwete Kinana haziwezi”
“Na
kama chama kupitia Halmashauri kuu yaani NEC wakiamua kumpitisha Kinana wajue
chama ndio kinachafuka na kuingia kwenye matatizo,kwani makada wasaka Urais
watatengeneza bifu kubwa kwa Kinana”alisema Seiph Yahaya msomi wa Masuala ya
Siasa kutoka chuo Kikuu cha Dodoma.
Kwa
mujibu wa Kada wa chama cha Mapinduzi Kutoka katika Umoja wa Vijana wa Chama
cha Mapinduzi UVCCM.ambaye naye akutaka kutajwa kwenye Mtandao huu alisema
Nguvu kubwa ya Kinana imetokana na msukumu mkubwa kutoka kwa Waziri Mkuu wa
sasa mizengo Pinda ambaye amekuwa akimbeza,Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward
lowassa kwamba hana sifa ya kuwa rais.
No comments:
Post a Comment