Wachokoza mada katika mdahalo huo ambao umemalizika muda mchache uliopita,mwanzo ni awadhi ally,Ayubu Rioba,Onesmo olenguruma,na Mwesiga baregu |
Na Karoli Vinsent
WANANCHI mbalimbali wamtaja Rais Jakaya
kikwete kuwa ni kikwazo kikubwa cha upatikanaji wa Katiba Mpya ,kutokana na
kushindwa kusimammia misimamo yake mwanzo ambayo ilikuwa inamalengo ya
kupatikana katiba mpya ya Wananchi.
Hayo,yamegundulika mda huu kwenye
Mdahalo wakujadili Katiba mpya,uliondaliwa na Umoja wa Asasi za kirai
(AZAKI)uliofanyika jijini Dar es Salaam,mdahalo huo ambao uliwahusisha Wananchi
wa Kawaida pamoja na Wasomi Mbalimbali.
Katika Mdahalo huo wananchi wameonekana
Dhahiri kumshutumu Rais jakaya Kikwete kwakushindwa kusimamia misimamo yake ya
mwanzo ambayo ilikuwa inalengo la kupatikana Katiba mpya ya
Wananchi bila Upendeleo,ambapo sasa ameonekana kubadilika na kuanza
kushikilia Misimamo yake ya Chama cha Mapinduzi CCM, ambayo inakuwa
kinyume na sasa.
Watanzania waliojitokeza katika mdahalo huo |
Kwa upande wake Msomi na mchambuzi wa
Masuala ya kisiasa Nchini kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Profesa
Mwisiga Baregu.alisema Rais kikwete amefanya usaliti mkubwa sana kwa wananchi
kwa kitendo chake kuanza kufuata maoni ya chama chake.
“Kiukweli mimi
sikutegemea Rais kikwete angefanya usaliti namna hii kwenye mchakato huu
wakatiba, wakati mimi sikutegemea .Kwanza wakati kila hatua tuliyokuwa
tunaifanya kwenye mchakato huu wakatiba tulikuwa tunamjulisha halafu na yeye
alikuwa anaungana na sisi kwa kazi tuliokuwa tuanafanya”
“Lakini tunashangaa yeye amebadilika na
kuanza kufuata misimamo ya chama chake,na huku ndiko alipoanza kuharibu
mchakato mzima wa ujio wa Katiba mpya.Alisema Baregu.
Baregu,ambaye ni Kada
kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,alizidi kusema kitendo cha
wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kutoka Chama cha Mapinduzi CCM.
Kuendelea kujadili
Rasimu ya Muundo wa Serikali mbili ni kuvunja kanuni ya mabadiliko ya katiba
kifungu cha 25,ambacho kinataka wajumbe wa Bunge hilo kutojadili Rasimu ya
Kwao.
Kwa Upande wake
Mwenyekiti wa Jukwaa la katiba Nchini,Deus Kibamba,aliwataka wananchi
kushirikiana na AZAKI ,kutetea katiba yao na kutowaacha wanasiasa kuhodhi
mchakato mzima wa Katiba.
Vilevile Mwanasheria
na mwenyekiti wa chama cha Wanasheria Zanzibar Hawadhi Ally, ambapo yeye
alikuwa miongoni mwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,alisema
Rais Jakaya Kikwete ndio mtu wa kulaumiwa kwa wananchi kwa kitendo chake cha
kuanza kufuata matakwa ya Chama chake ambao wamekuwa kinara wakubwa wakipinga
maoni ya tume ya Jaji warioba.
Mwenyekiti wa jukwaa la katiba tanzania Deus Kibamba akitoa maoni yake kama mwananchi katika mdahalo huo uliomalizika muda mfupi uliopita |
Naye Mwenyekiti wa
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali,inasimamia Muenendo wa Shuguli za Bunge
nchini,Marcus Albanile,aliwataka wananchi kuacha upole wa kuigopo Serikali ya
Rais Kikwete, ambayo imekuwa hikihalibu mchakato wa katiba mpya na
akawataka wananchi kuandamana na kulala barabarani na kudai katiba mpya.
Ikumbukwe, Midahalo
hii ya kuwapa wananchi fursa ya kujadili katiba mpya imeandaliwa na Umoja Asasi
zisizokuwa za Kiserikali AZAKI,ambao umoja huo unawakilisha Asasi hizo
zaidi ya mia tano.
No comments:
Post a Comment