Wamiliki, madereva na abiria wote mnatangaziwa kuwa kituo cha daladala Mwenge kitafungwa rasmi siku ya Jumapili jioni tarehe 01.06.2014. Kuanzia siku ya jumatatu asubuhi tarehe 02.06.2014 kituo kitakachokuwa kinatumika ni Makumbusho tu.
Sababu kubwa ya kufunga kituo hicho ni ufinyu wa eneo hilo jambo linalochangia dadalada kushindwa kuingia kituoni kwa wakati hasa vipindi vya asubuhi na jioni hivyo kusababaisha foleni kubwa katika eneo la Mwenge.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa eneo hilo kwa sasa litabaki kuwa eneo la wazi.
Madereva mnatakiwa kutii agizo hili ili kuepukana na hatua kali ambazo zitachukuliwa dhidi ya yeyote ambae atakaidi, aidha abiria mnatakiwa msilazimishe kushushwa eneo ambalo hakuna kituo cha daladala.
Barabara za kuingia na kutoka kituoni Makumbusho zinaendelea kukarabatiwa na Manispaa ya Kinondoni ili kusiwe na tatizo la kuingia kituoni hapo.
Conrad Shio
Afisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki
No comments:
Post a Comment