Mwenyekiti wa JUKATA DEUS KIBAMBA akizungumza na wanahabari mapema leo jijini dar es salaam |
Jukwaa
la katiba Tanzania JUKATA leo limetoa tathmini yake juu ya chaguzi mbili zilizofanyika katika
nchi za Malawi na Africa ya kusini mwezi uliopita huku wakionyesha kuipongeza
sana nchi ya Africa ya kusini kwa kufanya uchaguzi wa haki na huru tofauti na
nchi ya Malawi
Akizungumza
leo jijini dare s salaam mwenyekiti wa jukwaa
hilo DEUS KIBAMBA amesema kuwa wao kama jukwaa waliweka kambi katika
nchi hizo mbili,kwa lengo la kuangalia uchaguzi huo
Kaimu mwenyekiti wa jukata HEBRON MWAKAGENDA |
KIBAMBA
anasema kuwa ni wazi kuwa hali ya nchi hizo mbili kiuchumi ni tofauti sana
jambo ambalo pia limechangia kufanya chaguzi zao pia kutofautiana sana,ikiwa ni
pamoja na tume ya uchaguzi ya Malawi kuonyesha kuwa haikuwezeshwa kiswasawa
katika kusimamia uchaguzi huo jambo ambalo nchini Africa ya kusini halikuwa
hivyo.
“Tume
ya uchaguzi ya Africa ya kusini imeonyesha kuwajali sana wapiga kura hadi
kufikia hatua ya kuwajali walemavu ambao wasingeweza kufika vituoni na
kuwafwata walipo ili wapige kura.”amesema KIBAMBA
Kuhusu hamasa ya wananchi ya kupiga kura
JUKATA wamesema kuwa wananchi wa Africa ya kusini walikuwa na hamasa sana
tofauti na wale wa Malawi jambo ambalo limechangiwa na hamasa pia iliyofanywa
na serikali kwa ujumla.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini |
Akizungumzia
swala la rais wa Malawi kufuta matokeo
na kutangaza uchaguzi kurudiwa JUKATA
wamesema kuwa wameshangazwa sana na hali hiyo ambapo wameipongeza sana mahakama
ya nchini Malawi kwa kuonyesha ukakamavu wao katika kupingana na matakwa ya
rais banda na kuamuru matokeo yahesabiwe tena ambapo amesema kuwa kama hilo
lisingefanyika basin chi ya Malawi ingeingia katika machafuko makubwa sana.
No comments:
Post a Comment