Watanzania wametakiwa kuungana kwa pamoja katika
kuadhimisha siku ya mazingira duniani ambayo itaadhimishwa tarehe 5 mwezi juni
mwaka huu ambapo kidunia siku hiyo itaadhimishwa katika kisiwa cha BARBADOS
moja ya visiwa vya karibian na tanzania siku hiyo itaadhimishwa mkoani mwanza.
Akitangaza maadhimisho hayo leo mbele ya wanahabari
jijini dar es salaam waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais mazingira mh
BINILIUS MAHENGE amesema kuwa siku ya
mazingira duniani iliamuliwa na azimio la baraza la umoja wa mataifa la mwaka
1972 kama kielelezo cha ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa umoja wa mataifa
kuhusu mazingira uliofanyika huko stockholm nchini sweden.
Waziri mahenge amekiri mbele ya wanahabari kuwa
pamoja na siku hiyo kuadhimishwa kila mara hapa nchini lakini bado maeneo mengi
ya majiji hapa tanzania ni machafu sana huku akitolea mfano jiji la dar es
salaam ambapo limekuwa likiwa chafu kadiri siku zinavyozidi kwenda jambo ambalo
amekiri kuwa bado ni changamoto kubwa kwake na kwa ofisi yake.
Aidhia ametoa wito kwa watanzania wote kuadhimisha
siku hiyo ya mazingira duniani kwa vitendo kwa kuhakikisha kuwa wanafanya usafi
katika maeneo yao pamoja na kushirikiana na viongozi wao katika kufanya maeneo
yao kuwa masafi
No comments:
Post a Comment