KAMA ilivyotarajiwa, Michael Richard Wambura ameenguliwa katika kinyang’anyiro
cha Uchaguzi mkuu wa Simba SC unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao, kwa sababu
kubwa mbili.
Akizungumza katika Mkutano maalum na
Waandishi wa Habari mchana huu makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), makutano ya mitaa ya Ohio na Libya, Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati
ya Uchaguzi ya Simba SC, Wakili Dk Damas Daniel Ndumbaro amesema Wambura
ameondolewa kwa sababu kwa sasa si mwanachama halali wa klabu hiyo.
Wambura alisimamishwa uanachama wa
Klabu ya Simba tangu Mei 5 mwaka 2010 kutokana na kosa la kuipeleka klabu hiyo
mahakamani akifungua kesi namba 100 ya mwaka 2010 katika Mahakama ya Kisutu
mjini Dar es Salaam.
Ndumbaro amesema kuwa
Wambura aliwasilisha barua pia katika Kamati ya Uchaguzi akikiri kuipeleka
Simba mahakamani na kuiomba Kamati hiyo kumaliza suala lake na kuahidi
hatarudia tena kufanya kosa kama hilo, amepingana na Katiba ya klabu, TFF na
Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Mwenyekiti
huyo wa Kamati amesema kwamba pia walipokea barua mbili tofauti kutoka kwa
Wambura ya kwanza ikiwa ya Novemba 6 mwaka 2012 mgombea huyo akitaka kujua
uhalali wa uanachama wake na nyingine ya Septemba 15 ikijibu kuwa Simba haina
tatizo lolote na yeye.
“Kuna utata katika barua zake na pia kuna
barua ya tatu ya Septemba 25 mwaka 2012 ikieleza pia Simba hawana tatizo
na Wambura,” amesema Ndumbaro.
Aliongeza kuwa kutokana na Kamati yake
kujiridhisha na maelezo hayo, imeamua kumuondoa Wambura katika kinyang’anyiro
cha uchaguzi.
Ndumbaro ameeleza zaidi kuwa kutokana na
maamuzi ya kusimamishwa huko, Wambura hapaswi kushiriki katika shughuli za
Simba kwa mujibu wa Ibara ya 12(3) ya katiba ya klabu hiyo ya mwaka 2010 na
ibara ya 12(3) ya 2014.
Alieleza kuwa endapoa Wambura
hataridhika na maamuzi hayo anaruhusiwa kukata rufaa kwenye Kamati ya Maadili
ya TFF.
Ndumbaro amesema pia wagombea wengine wote walioekewa pingamizi wamepitishwa na wataendelea na mchakato wa uchaguzi huo utakaofanyika Juni 29 mwaka huu.
Ndumbaro amesema pia wagombea wengine wote walioekewa pingamizi wamepitishwa na wataendelea na mchakato wa uchaguzi huo utakaofanyika Juni 29 mwaka huu.
Kwa kuondolewa Wambura, nafasi ya wagombea
Urais inabaki na watu wawili, ambao ni Evans Elieza Aveva na Andrew Peter Tupa,
wakati wanaowania Umakamu wa Rais ni Jamhuri Kihwelo, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’,
Joseph Itang’are ‘Kinesi’ na Swedi Nkwabi.
Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo,
Wambura amesema kwamba atazungumza kesho katika Mkutano na Waandishi wa Habari,
kwa leo hakuwa tayari kuzungumza na mtu mmoja mmoja.
No comments:
Post a Comment