Kufuatia kuibuka kwa mgogoro wa ardhi hapa nchini diwani wa
kata bunju amekanusha tuhuma za kuhusika na ugawaji wa ardhi katika jimbo lake
kinyume na sheria nakusisitiza kuwa yeye sio muhusika wa ugawaji wa ardhi ambao
umegharimu shilingi milioni miatatu.
Akizungumza jijini dare s salaam diwani kata hiyo
Maji Masafi Sharifu amesema tuhuma zilizotolewa nabunge wa kawe Halima Mdee si
za kw eli nakusisitiza kuwa kama anao ushahidi wa ugawaji wa ardhi kinyume na
sheria mbunge huyo anatakiwa kwenda makamani ili kuthibitisha tuhuma zilizo ibuliwa na mbunge
huyo wa kawe tiketi ya chadema .
‘’kama imebainika kama nimechukua hizo fedha
ninamuomba mheshimiwa mdee aende akaithibitishie mahakama juu ya tuhuma alizo
nituhumu na kama itabainika ni kweli nitajiuzulu wa wadhifa wangu kama diwani
wakata ya bunju kwani ninazo njia nyingi za kutafuta pesa’’Alisema Maji masafi.
Maji masafi alisema kumekuwa na kundi ambalo
linajulikana kama mungiki ambalo limekuwa likiongozwa na mbunge huyo wa kawe
Halima mdee ambapo limekuwa likitoa kauli chafu dhidi yake ,aidha kundi hilo limekuwa
nania yakumchafua diwani huyo kwa malengo ya kisiasa.
Alisema kundi hilo linalojukana kama mungiki
limekuwa nawatu thelathini na tano limekuwa likishinikizwa na mbunge huyo kuwa
ndiye aliye chukua fedha hizo.
‘’tumekuwa tukisaidiana sana lakini kumekuwa
nakundi dogo linalo jiiita mungiki limekuwa likishinikizwa na mbunge Halima
kuwa mimi ndiye nilihusika naugawaji waviwanja katika kata hiyo yabunju.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa kitongoji
cha basi haya Danel Aron katika kata hiyo amesema kuwa mbunge wa kawe amekuwa
akimtuhumu kuwa ndie anaye gawa ardhi katika kata hiyo jambo ambalo mwenyekiti
wa kitongoji hicho amekanusha.
Daniel Aron alisema kutokana na tuhuma hizo
kumekuwa ujumbe mzito unatumwa kwenye simu zake zikiwa zikimtishia maisha
mwenyekiti huyo .
‘’tumekuwa tukipokea meseji za vitisho huwezi
kutafuta umaarufu wa kisiasanaomba muheshimiwa mumulize kama anauthibitisho
‘’Alisema Aron.
Kiongozi wa kata hiyo Elikimu mwaipaya amesema
kuwa wamekuwa wakishangazwa na mbunge huyo angetakiwa kulifuatilia swala hilo
lakini mbungehuyo amekuwa akiwaerudisha nyuma.
No comments:
Post a Comment