Baada ya mtandao huu wa HABARI24 kupokea na kusikia malalamiko ya wafanya biashara na wananchi wengi juu ya kituo cha polisi cha msimbazi kilichopo kariakoo jijini dar es salaam ambapo wanakishutumu kwa kuwakamata hovyo hovyo wafanyabiashara wa matunda na bidhaa nyingine pamoja na wateja wao na kuwapiga na kuwapeleka kituoni hapo kwa kuwalipisha faini bila hata ya kutoa risiti
Mtandao huu jana ijumaa uliamua kuweka kambi jirani na kituo hicho cha polisi ambapo watu zaidi ya 30 wakiwemo wauza matunda na wateja wa matunda hayo walikuwa wamekamatwa maeneo mbalimbali ya soko hilo la kariakoo jambo ambalo liliwashangaza wengi kuona hadi wateja wa bidhaa hizo wanakamatwa na kupigwa na kuteshwa sana kama wao ndio wauzaji wa matunda katika maeneo hayo ya kariakoo.
Nikiwa maeneo ya kariakoo nilishughudia watu waliokuwa wanaletwa na gari la polisi katika kituo hicho cha msimbazi ambapo katika watu hao kulikuwa na dada mmoja aliyejitambulisha kwangu kwa majina mawili ya RAHAB MBISE ambapo katika hali isiyokuwa ya kawaida alionekana kutokubaliana na maamuzi ya polisi ya kumpiga na kunyanyasa akiwa amechanganywa na wauzaji wa matunda ambao wao walikuwa wamekamatwa kwa kosa la kuuza matunda katika maeneo ambayo sio rasmi.
Baada ya watuhumiwa hao kuingia ndani nilitaka kujua kile ambacho kilikuwa kinaendelea ndani juhudi ambazo ziligonga mwamba ikanilazimu nisubiri nje ili baada ya hao watuhumiwa kutoka wanisimulie kile ambacho wamekifanya ndani ya kituo hicho.
Nikiwa nje ya kitui hicho cha polisi cha msimbazi kariakoo watuhumiwa walianza kutoka ambapo yule dada aliyekuwa akipigwa sana na askari hao huku akionekana wazi sio muuzaji wa bidhaa yoyote ni mpita njia na mteja tuu nilifanikiwa kuongea naye,kisa cha kuteswa kwa huyu dada ni kutaka kupokea siku yake iliyokuwa inaita ndio wakamtuhumu kuwa anawapiga polisi hao picha.
HAPA SIKILIZA KISA KILICHOMFANYA AKAMATWE NA ASKARI HAO AMBAO WALIKUWA HAWANA HATA SARE YA JESHI LA POLISI--
Moja kati ya mambo ambayo yanalalamikiwa sana katika kituo hicho ni rushwa kubwa sana iliyokidhiri.SASA SIKIA RUSHWA ILIVYOTEMBEA NDANI YA KITUO HICHO NA AFANDE MMOJA AMBAYE TUMEPATA JINA LAKE MOJA AFANDE HAPPY AMEHUSISHWA SANA NA KUWATESA KUWATUKANA NA MWISHOWE KUWACHANGISHA HELA WATUHUMIWA HAO BILA HATA YA KUWAPA RISITI.
Kituo hicho kimekuwa kikilalamikiwa sana na wafanyabiashara wa kariakoo kwa kufanya unyanyasaji kwao na kupokea rushwa pindi wanapowapeleka katika kituo hicho.
JITIHADA ZA KUWATAFUTA WAHUSIKA ZINAENDELEA.
No comments:
Post a Comment