Chama cha wananchi CUF leo kimeanza rasmi mkutanmo mkuu wa chama hicho ambapo pamoja na mambo mengine chama hicho kitafanya uchaguzi wa viongozi wake wa ngazi za juu.
Akizungumza na mamia ya wanachama wa chama hicho mwenyekiti wa CUF IBRAHIM LIPUMBA amesema kuwa chama hicho kijiandae kufanya uchaguzi wa makini ili kupata viongozi ambao watasaidia katika kupata ushindi katika uchaguzi ujao nchini
Akizungumzia swala la katiba na UKAWA kutoka nje amesema kuwa kamwe UKAWA haitakufa,na hawapo tayari kurudi tena bungeni kama wana CCM hawataaxha kujadili rasimu yao na kujadili rasimu ya wananchi kama ilivyopelekwa bungeni,huku akimtaka Rais KIKWETE kuunusuru mchakato huo ulipokwama.
Katika mkutano huo wa mwaka wa CUF umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa akiwemo mwenyekiti wa CHADEMA FREEMAN MBOWE na katibu wake DK WILBROD SLAA.
Ishara ya serikali tatu ndio ilmetawala katika mkutano huo ambapo kila kiongozi aliyesimama alikuwa akiwataka wanachama kusema ni serikali tatu pekee |
Makamu mwenyekiti wa CCM BARA PHILIP MANGULA ameiwakilisha CCM katika mkutano huo ambapo katika salamu zake ameonekna kuwapongeza CUF kwa kuwa chama chenye misimamo |
SAWA SAWA--katibu mkuu wa CUF akizungumza na wajumbe hao katika mkutano huo |
Picha ya pamoja |
Katibu mkuu wa CHADEMA akiwa na katibu mkuu wa NCCR mageuzi mosena nyambabe HABARI ZAIDI KUHUSU MKUTANO HUU ZITAKUWA ZINAKUJIA HAPA HAPA |
No comments:
Post a Comment