Jeshi la Polisi Kanda Maalum limeanza
uchunguzi cha kuhusu tukio la moto mkubwa uliotokea katika soko la Mchikichini Ilala.
Tukio hilo lilitokea ghafla majira ya
saa tano za usiku ambapo bidhaa mbali mbali za wafanyabiashara ziliteketea kwa
moto. Watu walioshuhudia tukio hilo
waligundua motu huo ulianzia katikati ya soko.
Licha ya juhudi kubwa zilizofanywa na kikosi cha Zimamoto na Shirika la
Umeme Tanesco bado moto huo ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kuteketeza sehemu
kubwa ya soko.
Jitihada kubwa sana zilifanywa na Kikosi
cha Zimamoto na kutoka Jiji, Bandari pamoja na kampuni Binafsi zenye magari ya
Zimamoto. Hali ilikuwa ngumu sana
kulingana na bidhaa zilizokuwa zinaungua ikiwa ni pamoja na nguo, viatu, mabegi
na vifaa vya plastiki ambao zilichochea moto huo kuenea kwa kasi.
Kazi kubwa iliyofanyika ilikuwa ni kuzuia moto
huo usisambae katika makazi ya watu jambo ambalo lililokuwa gumu lakini
liliwezekana kupitia watendaji hapo juu.
Jeshi la Polisi lilidhibiti wizi au
upotevu wa mali na wahusika walijulishwa wakafika na hata wale wakorofi
walidhibitiwa. Baada ya jitihada kubwa
ya ziada moto huo ulizimwa majira ya saa 9.00 usiku huku ulinzi ukiimarishwa
hadi asubuhi ya leo. Aidha hakuna
taarifa zozote za watu waliopoteza maisha au kujeruhiwa.
Mizigo yote iliyookolewa haikuruhusiwa
kuondolewa eneo la tukio ili kusubiri uthibitisho wa wanaohusika. Mpaka sasa haijafahamika chanzo cha moto huo
na kwa kushirikiana na vikosi vyote tajwa hapo juu uchunguzi umeanza mara moja
ili kujua chanzo halisi cha moto huo ikiwa ni pamoja na kutumia wataalamu wa
kimaabara (Forensic Investigation).
Taarifa kamili
itatolewa mara baada ya kukamilika kwa moto huo.
No comments:
Post a Comment