Katika tukio la kwanza, Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaa limefanikiwa kuwakamata watu watatu kwa tuhuma za kupatikana na vipande 26
vya meno ya Tembo kinyume cha sheria.
Tukio hili lilitokea tarehe 29.05.2014 huko maeneo ya M’nyamala
Kata ya Mwinyijuma Osterbay (M) Kinondoni baada ya kupata taarifa toka kwa msiri kuwa kuna gari
namba T 178 BSY NOAH inasemekana ina
mizigo ya wizi.
Baada ya taarifa hizo askari walijipanga na
kuweka mtego na kufanikiwa kulikamata gari tajwa hapo juu na walipolipekuwa
walikuta viroba viwili vilivyokuwa na vipande hivyo vya meno ya tembo ambavyo
thamani yake haikufahamika mara moja.
Watuhumiwa pamoja na gari husika
vinashikiliwa.. Watuhumiwa hao ni kama ifuatavyo:
· ADAM S/O YONA,
miaka 37, mkazi wa Mbagala,
· SELEMANI S/O LEONALD,
Miaka 37, Mkazi wa M’nyamala,
· HUSSEIN S/O SAID,
Miaka 34,
Katika tukio la pili, mnamo 05/06/2014 Polisi Wilaya ya Buguruni mkoa wa
kipolisi Ilala kwa kushirikiana na bwana BAKARI S/O YUSUF, Miaka 33, Mhifadhi
Wanyamapori Makao Makuu, Mkazi wa Mbezi Beach, walifanikiwa kukamata vipande 28
vya meno ya Tembo vyenye thamani ya Tshs 275,550,000/= nyumbani kwa DOMINICK S/O
KOLINELI @ KOMBE, Miaka 35, Mkazi wa Tabata Kisukuru.
Walipofanya upekuzi katika nyumba hiyo ambapo kwenye
chumba kimoja cha uwani cha bwana HERBERT
S/O REVIL MACHAKA, Miaka 30, mkazi wa Morogoro, ambapo kilipatikana kipande 1
cha jino la Tembo. Upekuzi uliendelea kwenye Stoo na Jiko na walipata vipande 27 vya meno ya tembo na
kufanya jumla ya vipande hivyo kuwa 28. Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa ili
kubaini mtandao mzima wa ujangiri huu unaomaliza rasilimali za taifa.
No comments:
Post a Comment