Na Karoli
Vinsent
KAULI aliyoisema Waziri Mkuu
aliyejiuzulu Edward Lowassa kwamba
vijana wasiokuwa na Ajira ni Bomu
linalosubiri kulipuka muda wowote,linazidi kujidhihirisha, Baada ya leo Maofisa wa Uhamiaji
kuonja kali ya mwaka, ambayo
hawataisahau maishani mwao.
Hayo yalibuka leo Kwenye Usahili wa Vijana ambao waliomba nafasi ya
kujiunga Jeshi la uhamihaji nchini kwa mwaka
huu,ambazo zilifanyika kwenye uwanja mpira wa Taifa Jijini Dar es Salaam,ambapo vijana hao walikuwa wengi na kujaza uwanja huo kama kuna mechi ya mpira ya
Watani wa jadi Simba na Yanga,ambayo imekuwa ikijaza watu kiasi hicho.
Mwandishi wa Mtandao huu, alifika eneo hilo ndipo alishudia kundi la watu
likiwa likisubili kufanyiwa usahili,huku vijana hao wakiwa wamechoka kwa kuwangojea maofisa hao
ili waje kuwapa mitahani ambayo wanaitumia kwenye usahili.
Ambapo vijana hao wakitoa malalamiko kwa maofisa hao wa uhamiaji kwa kuwa
weka kwa mda mlefu.
“Kama wanachakachua hayo majina waseme tu,maana tumekaa mda mrefu sana hapa, akuna
chochote kinachofanyika”alisema kijana mmoja ambaye aligoma kutaja jina lake
mtandaoni
Kwa upande wake kijana mwengine aliyetambulika kwa Jina Moja la Juma naye
alionekana kupata wasiwasi kuhusu upatikanaji wa ajira hiyo kwenye jeshi hilo ambalo ni la
muhimu katika Taifa letu.
“Jamani hivi mimi sina bahati na soko hili la Ajira la Tanzania
nimezunguka na vyeti vyangu zaidi ya miaka miwili nakosa kazi hivi haka
“kadegree” yaani Shahada yangu ina nini jamani mbona nateseka hivi”alisema Juma
Mwandishi
wa Mtandao huu alipotaka kupata ukweli kutoka kwa maofisa hao wa Jeshi la
Uhamiaji kuhusu shutuma hizo,ambapo alijitokeza Ofisa mmoja ambaye akutaka
kutaja jina lake kwa kusema yeye sio Msemaji wa Jeshi la Uhamiaji.
“Hatuna Jinsi sisi ndugu mwandishi,kumbukeni pia na sisi binadamu hebu wewe ungekuwa
kuwa sisi ungefanyaje,maana watu ni wengi sana nchi hii hawana Ajira,na
tumefanya kazi kubwa sana kuwapunguza”
“Kwani watu waliomba zaidi ya Laki mbili,tena tumewapunguza mpaka
wakamebaki kiasi
ambacho tunaweza kukimudu,na hawa wenyewe unaowaona tumewagawa kimakundi
wengine wamekuja leo
“Ijumaa”na wengine tumewapangia tarehe 16 mwezi huu,hali ni mbaya sasa
kaka Ajira hakuna watu wanachanganyikiwa tu hao”alisema ofisa huyo
Mwandishi
alipotaka kujua
nafasi hizo ambazo idara hiyo ni watu wangapi,ofisa
huyo alisema waitaji watu 250.
Uchunguzi
wa Mwandishi wa Mtandao huu,umebaini idadi ya watu waliofika tu kwenye usahili
wa kwanza ni zaidi ya elfu ishirini huku kukiwa na hatua nyingine ya usahili itakayofanyika jumatatu
ijayo,ambayo nayo itakuwa na watu wengi zaidi ya hiyo.
Vijana hao waliojitokeza kwenye usahili huo, ni miongoni mwa waliomaliza kutoka vyuo vikuu
mbalimbali nchini,ambao wanye ngazi ya elimu kwaanzia Diploma hadi shaada ya
pili .
Naye msomi na mchambuzi wa Masuala ya Kisaisa kutoka chuo Kikuu cha
Dodoma,Seiph Yahaya alisema kwa sasa Serikali inahaja ya kutafakali kauli ya
aliyoisema Edward Lowassa,kuhusu kauli yake ya ukosefu wa Ajira kwa vijana.
“Kikuweli mimi nakwambia hili ni Bomu tu linalosubili kupasuka mda wowote tu,sahivi
hali ni mbaya sana hususani linapofikia suala la Ajira inakuwa balaa na yote
haya ndugu yangu ni Makosa yalifanywa na Serikali hii,haiwezekani wamalize
Viwanda vyote kwa kuviua”
“utategemea nini sasa,kama serikali ingewekeza kwenye viwanda vyandani sidhani tatizo lingekuwa
kubwa kama sasa kama hivi ilivyokuwa kubwa,na lazima hili litakuwa Bomu
tu”alisema Seiph Yahaya
No comments:
Post a Comment