WATUMIAJI wa simu za kisasa za Smart Phone wametakiwa kutumia chaji za Puku kuchajia simu zao ili kujihakikishia usalama wake. |
Akizungumza na waandishi wa habari
katika uzinduzi wa chaji hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya PUKU alisema
kuwa chaji hizo kwa sasa zinapatikana hapa nchini.
Alisema kuwa ni chaji ambazo zinahifadhi
umeme kwa muda mrefu ambao unakuja kutumiwa kuchajia simu hasa pale ambapo
panakuwa hakuna umeme.
Aliongeza kuwa bei yake kwa sasa ni
kuanzia 160,000 kutokana na ubora wake na pamoja na namna ambavyo inasaidia.
"Mimi ni mtanzania kutoka Tanga na
nilisoma hapa hapa ila nilielekea Marekani kusoma na ninaishi huko na nimebuni
hii chaji kwa lengo la kusaidia watu mbalimbali ambao wanakuwa wakisumbuliwa na
tatizo la kuchajia simu zao pale ambapo panakuwa hakuna umeme wa
uhakika"alisema Meck Mbwana ambaye ni mvumbuzi na mkurugenzi mtendaji wa
PUKU.
Hiki ndicho kifaa ambacho unaweza kukitumia katika kuchaji simu yako muda na mahali popote ulipo sasa kinapatikana tanzania |
Aliongeza kuwa " kumekuwa na
ongezeko kubwa la matumizi ya simu za smart phone huku watumiaji wakilalama
kuwa wanakosa uhakika wa umeme wa kuzihudumia sasa hii bidhaa itasaidia".
Aliongeza kuwa kwa sasa zinapatikana
hapa nchini na aliwataja wahusika wakubwa kuwa ni pamoja na Ed Kavishe-mshirika
mwenza, Joseph sikare – Rais Tanzania huku Mwanamitindo Millen Magese akiwa ni mshirika
mwenza na balozi wao.
Lucy T. Ngongoseke, Managing Director, Tabasamu Pr Consultancy |
The CEO wa puku MECK MBWANA |
Tayari PUKU wameshajikita na uchangiaji
wa huduma kwa jamii ambapo asilimia kadhaa ya mauzo itaelekezwa kwenye kampeni
ya uelewa wa hali ya endometriosis na ujenzi wa hospital kwa ajili ya magonjwa
yanayowasumbua akina mama.
JOSEPH SIKARE ambaye ni raisi wa PUKU tanzania akizungumza |
Mbali na udhamini wa kampeni ya
endometriosis PUKU watachangia ujenzi wa madarasa mawili yaliyoko chini ya
mradi wa Millen Magese Foundation yanayojengwa huko Mtwara ambapo mpaka sasa
madarasa matatu yameshakamilika.
No comments:
Post a Comment