IKIWA imebakiza mwaka mmoja tu,ili
kufikia uchaguzi mkuu mwaka 2015,nacho chama cha Demokrasia na Maendeleo
CHADEMA,kimeingia katika mgogoro mwingine baada ya baadhi ya wanachama wake
kuibuka leo na kudai ndani ya chama hicho kuna ufisadi unaoendelea.
Hayo,yaligundulika leo Jijini Dar es
Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi Habari na Viongozi wa chama hicho kutoka
mikoa mbalimbali,ambao wanafikia 78 vilevile Viongozi hawo ni Wajumbe wa Baraza
kuu na mkutano mkuu wa CHADEMA.
Akisoma maazimio ya viongozi hao,Katibu
wa chadema mkoa wa Tabora Athumani Balozi,alisema wamefikia hatua hii kupingana
na viongozi wa Juu wa Chama hicho ni kutokana na kile wanachodai ni
Kuchoshwa na Vitendo
vya Ufisadi vinavyofanywa na viongozi wakuu wa chama hicho.
“Matendo ya viongozi wetu ni Unafiki wa Kisiasa
,kiasi cha kutumia Mabilioni ya chama kwenda kummaliza kisiasa
kiongozi mwenzao Zitto Kabwe na kuacha ujenzi wa Chama ukiendelea kuporomoka”
“Kwenye ujinga huu,hakuna wa kumlahumu
zaidi viongozi wetu wenyewe”alisema Balozi
Balozi,ambaye ni mjumbe wa Baraza la
Mashauriano Kanda ya Magharibi wa CHADEMA,alizidi kusema chama kina endeshwa
kifisadi kwani fedha za Ruzuku kutoka kwenye chama hicho, zinakwenda kwenye
mifukoni mwa Mwenyekiti wa chama hicho .
“Tunasikitishwa sana na Kitendo cha
Mwenyekiti wa Mbowe kusema anajilipa madeni aliyokikopesha chama kila
siku,kiasi cha Millioni 700 ,sasa tunashindwa kuelewa deni hili ni deni gani
lisiloisha?”
“Na je deni hili alikikopesha chama kwa
mkataba gani?na mbele ya nani huo mkataba wa mkopo?taratibu za chama chama za
Kukopa za fedha zilifuatwa au matumizi mabaya ya Fedha za Umma”alizidi kusema
Balozi.
Kuhusu mbowe kununua Magari chakavu ndani chama hicho.
Katibu huyo,Athumani
Balozi alisema mbowe anafaa kutokubalika ndani ya chama hicho kutokana na
kufanya utapeli wa kununua Magari chakavu ambayo yanafikia Milioni 700,huku
akijua ni chakavu na kwamba kabla ya kukiuzia chama alikuwa anayakodisha magari
hayo.
Vilevile ,alizidi kusema wao wamebaini
Mbowe kanunua Landcruiser V8 VX 2 kwa pesa za Chama hicho,tena magari mengine
ndani ya chama hicho yamesajiliwa kwa jina la MBOWE HOTELS ,huku akijua kufanya
hivyo matumizi mabovu ya Fedha.
Kuhusu CHADEMA kususia vikao vya Bunge
Maalum la Katiba.
Naye, Mwenyekiti wa
Chadema Mkoa wa Temeke ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama hicho
Joseph Yona ,alisema kitendo hicho cha ni kuvunja kanuni za chama
hicho.
“Bunge la Katiba lilikuwa ni mazao ya
juhudi zetu sisi wanachadema tuliopambana nchi nzima kuidai katiba”
“Nashangaa leo chama hichi kimeunda
baraza kivuli la Mseto na Vyama tulivyowaaminisha watanzania kuwa vina ushiriki
na CCM,huku bila hata kutushirikisha wajumbe wa Baraza la mkutano mkuu,huku
wakijua wanaojiunga nao ni CCM B”alisema Yona.
Yona,ambaye ni mwenyekiti pia Vijana wa
Chama hicho mkoa wa Temeke,alizidi kusema chama cha Wananchi CUF pamoja na NCCR
na kujiundia umoja unaojiita UKAWA.ni unafiki ambao unakimaliza chama hicho
kwani vyama hivyo vinaubia na Chama cha Mapinduzi CCM.
No comments:
Post a Comment