Kaimu mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Bw HAROLD SUNGUSIA akizungumza na wanahabari muda mchache uliopita |
Ikiwa leo bara la Africa linaadhimisha siku ya mtoto
wa Africa kituo cha Sheria na Haki za binadamu Tanzania LHRC kimesema kuwa bado
serikali ya Tanzania haijaonyesha dhamira ya dhati katika kulinda na kuheshimu
haki za mtoto wa kitanzania kama ilivyo katika mataifa mengine .
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu bw HAROLD SUNGUSIA wakati wa
mkutano na wanahabari alipokiwa akitoa tamko la kituo hicho juu ya siku hii ya
mtoto wa Africa ambapo amesema kuwa pamoja na jitihada zilizofanywa na serikali
ikiwemo kuundwa kwa sheria ya mtoto ya mwaka 2009 na kuridhia mikataba
mbambali ya kimataifa bado mtoto wa
kitanzania anakabiliwa na changamoto nyingi ambazo bado serikali imeshindwa
kuzitatua.
Akitaja matukio ambayo mablimbali ya ukiukwaji wa
haki za mtoto ambayo yanamkuta mtoto wa kitanzania amesema kuwa matukio kama
,kubaguliwa,kunyanyapaliwa,kubakwa,kulawitiwa,kudharauliwa,kufanyishwa kazi za
ndani,na kunyanyaswa,pamoja na tabia ya wazazi kuwatuma watoto wao vileo mbalimbali ni matukio machache
ambayo bado yanamtokea mtoto wa kitanzania huku serikali ikishindwa kuyamaliza
matatizo hayo.
Bw SUNGUSIA ametolea mfano tatizo la kulawitiwa
ambapo amesema kuwa kwa mwaka jana tu watoto zaidi ya mia nane walirepotiwa
kulawitiwa idadi ambayo ni kubwa sana kwa nchi kama Tanzania,huku akiitaka
serikali kuhakikisha inalivalia njuga swala hilo kwani limeanza kuota mizizi.
Wanahabari wakiwa makini kumsikilza |
Aidha kituo cha sheria na haki za binadamu wamesema
kwa kuheshimu umuhimu wa mtoto katika bara letu la Africa na nchi yetu ni
lazima kuheshimu na kuzingatia sheria za nchi zinazomlinda mtoto,elimu ya haki
ya mtoto itolewe pamoja na kila mtu kuwajibika katika kumlinda mtoto katika kuhakikisha
uhuru wa mtoto unapatikana.
Siku ya mtoto wa Africa inaadhimisha kila siku barani Africa kuwakumbuka watoto waliouawa
huko Africa ya kusini wakiwa katika maandamano ya kudai haki na usawa wa elimu
katika kitongoji cha Soweto mwaka 1976
No comments:
Post a Comment