|
BAJETI MBADALA YA
KAMBI YA UPINZANI 2014/2015
|
BAJETI YA SERIKALI
KWA MWAKA 2014/2015
|
1
|
Bajeti isiyo na
Mikopo ya kibiashara hivyo bajeti inalenga kulipunguzia taifa mzigo wa
madeni.
|
Bajeti ya Serikali
ina mikopo yenye masharti ya kibiashara ya shilingi trilioni 4.3 na hivyo
bajeti hii inawaongezea wananchi mzigo wa madeni.
|
2
|
Bajeti inayoendelea
kusisitiza umuhimu wa kuwalipa pensheni wazee wote nchini wenye umri wa miaka 60 na kuendelea.
|
Bajeti ya Serikali
iko kimya kabisa kuhusu malipo ya pensheni kwa wazee wote nchini.
|
3
|
Bajeti inayoendelea
kusisitiza kushusha kiwango cha tozo
ya kodi ya mapato ya ajira kwa wafanyakazi (PAYE) hadi kufikia asilimia 9.
|
Bajeti ya Serikali
imeendelea kuwakandamiza wafanyakazi kwa kutoza asilimia 12 ya kodi ya mapato ya ajira (PAYE) kwa wafanyakazi.
|
4
|
Bajeti ya Upinzani
imeainisha vyanzo vipya vya mapato ya
ndani na hivyo inayojitegemea kwa
asilimia 84.38
|
Bajeti ya Serikali
ni tegemezi kwa asilimia 36.4 kutokana
na kukopa kwa kiwango kikubwa na hivyo
kuongeza deni la taifa.
|
5
|
Bajeti Mbadala,
mapato ya ndani ni asilimia 34.55 ya pato la Taifa
|
Bajeti ya Serikali,
mapato ya ndani ni asilimia 23 ya pato la taifa.
|
6
|
Bajeti inayolenga
kupunguza misamaha ya Kodi hadi kufikia asilimia 1 ya Pato la Taifa ili
kuongeza mapato ya ndani.
|
Bajeti ya Serikali
imetaja tu azma ya kupunguza misamaha ya kodi lakini haijataja ni kwa
asilimia ngapi ya pato la taifa wala haijaainisha watakaofutiwa misamaha
hiyo.
|
7
|
Bajeti
inayolenga kutekeleza kikamilifu
miradi ya maendeleo kwa kutenga asilimia 42.67 ya bajeti yote
kugharamia miradi ya maendeleo.
|
Asilimia
22 ya Bajeti yote ya Serikali
inakwenda kulipa deni la Taifa na asilimia 67.5 ni matumizi ya kawaida. Hivyo miradi ya
maendeleo haijapewa kipaumbele.
|
8
|
Bajeti
inayolenga kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo ambavyo havimuumizi
mwananchi wa kawaida
|
Bajeti
ya Serikali imelenga kukusanya mapato kutoka katika bidhaa zinazotumiwa kila
siku na wananchi kama vile vinywaji na hivyo kuwaongezea wananchi ugumu wa
maisha.
|
9
|
Matumizi
ya Kawaida ni asilimia 57.33 tu ya bajeti yote
|
Matumizi
ya Kawaida ni 67.5%
|
10
|
Bajeti
ya kumsaidia mwananchi wa kawaida kutoka katika wimbi la umaskini.
|
Bajeti
isiyo mtambua mwananchi maskini na kuongeza matumizi makubwa kwa watawala.
|
|
|
|
No comments:
Post a Comment