Wednesday, June 11, 2014

NENO LA MICHAEL WAMBURA BAADA YA KAMATI YA RUFANI KUMRUDISHA KWENYE UCHAGUZI WA SIMBA SC

Michael Richard Wambura amemfunga bao tamu mwanasheria Dkt. Damas Ndumbaro baada ya kamati ya Rufani ya TFF kumrudisha, sasa vita ni kati yake na  Evanc Aveva kwenye king`anyiro cha Urais katika uchaguzi wa juni 29 mwaka huu. 

SAA chache baada ya kamati ya Rufani ya shirikisho la kandanda Tanzania, TFF, chini ya mwenyekiti wake, Wakili Julius Mutabazi Lugaziya kumrudisha, Michael Richard Wambura kwenye uchaguzi wa Simba sc, mgombea huyo amesema sasa haki imetendeka na uchaguzi utakuwa wa amani.
Wambura amezungumza na mtandao huu dakika chache zilizopita na kusema kuwa anaufananisha ushindi wake kama mchezo wa mpira wa miguu.

No comments: