Mkurugenzi mkuu wa tigo DIRGO GUTIEREZ akizungumza na wanahabari leo wakati wa utiaji saini huo muda mfupi uliopita |
Kampuni ya simu za mikononi Tanzania ya Tigo leo imeingia katika ushrikiano na Dar Teknohama Busness incubator DTBI ambayo itaona kampuni hiyo ya simu ikiwezesha washiriki wa teknohama kukuza vipaji vyao kupitia mpango maalum wa mafunzo na biashara ambayo itasaidia kukuza ajira nchini kupitia taaluma hii ya teknohama.
Akizungumza kuhusu ushirikiano huo katika makao makuu ya tume ya sayans na taknologia jijini dar es salaam,mkurugenzi mkuu wa tigo DIEGO GUTIEREZ amesema kuwa ushirikiano huo na DTBI utawapatia watanzania ambao ni wanasayans wa baadae fursa ya kujifunza na kuendeleza vipaji vyao huku biashara inayotokana na teknologia ikizidi kukua na na kuchangia suluhu za kidigitali katika jamii.
Waziri wa sayans,mawasiliano na teknoligia Profesa MAKAME MBARAWA akizungumza |
Amesema kuwa kuwa hadi sasa teknoihama inachangia asilimia 2.3 katika GDP ya nchi ambapo amesema kuwa tigo ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha kuwa kiasi hicho kinakua kupitia uwekezaji wa rasilimali watu.
Aidha amesema kuwa tigo kwa kuhakikisha kuwa malengo yao yanafanikiwa wametangaza kutoa ahadi ya kuwasomesha wanafunzi kumi katika ngazi ya shahada ya uzamili kila mwaka pamoja na kutoa nafasi ya mafunzona nafasi za ajira kwa wale ambao wamejikita katika masomo katika masomo ya ya Teknohama.
mkurugenzi mkuu wa tigo DIEGO akibabidhiana mkataba na afisa mtendaji mkuu wa DTBI enginer GEORGE MULAMULA KATIKA HAFLA HIYO |
Utiaji saini huo ulishughudiwa na waziri wa mawasiliano sayansi na technonogia PR MAKAME MBARAWA ambaye ameipongeza sana kampuni ya tigo na DTBI kwa kuingia katika ushirikiano huo.Amesema kuwa serikali inayofuraha kubwa sana kuwaunga mkono katika ushirikiano huo ambao utaendelea kuwawezesha vijana na wajasiriamali wa technologia kupata maarifa na msaada katika kukuza ubunifu wao ili kuweza kusindana kikamilifu katika soko la biashara siku za usoni.
Tunasaini |
Akizungumza katika uzinduzi wa ushirikiano huo afisa mtendaji mkuu wa DTBI enginer GEORGE MULAMULA amesema kuwa ushirikiano huu utawapa washiriki fursa mbalimbali kuonyesha vipaji vyao kitaifa na kimataifa
No comments:
Post a Comment