HAPPYNES MILLEN MAGESE jina hili sio adimu sana
masikioni mwa watanzania walio wengi,huyu ndiye aliyewahi kuwa miss Tanzania mwaka
2001 na kujizolea umaarufu wake hapa nchini na nje ya Tanzania.
Pamoja na kuwa miss Tanzania mrembo huyu amebahatika
kuwa na kipaji cha uwana mitindo kipaji ambacho kimempa mafanikio makubwa hata
kumpa umaarufu wa dunia kwa shughuli hiyo ya uwanamitindo.
Mrembo huyu baada ya kufanikiwa kuwa miss Tanzania alifanikiwa
kuhamia nchini Africa ya kusini ambako alianza kufanya kazi zake za uwana
mitindo na kujizolea umaarufu mkubwa sana na baadae kuishi pia nchini marekani
kwa ajili ya kazi hiyo hiyo
Historia ya binti huyu ni kubwa sana kwani ni moja kati ya
warembo wa Tanzania waliotumia vizuri nafasi walizopata kwa ajili ya
kujiendeleza na kupata mafanikio
Kabla ya MILLEN kuwa miss Tanzania akiwa na umri wa
miaka 15 tu alianza kupata tatizo ambalo lilikuwa linamkosesha raha sana tatizo
ambalo kwa hapa Tanzania walishindwa kujua nini kinamsumbua hasa,kwani alikuwa
akipata maumivu makali wakati wa hedhi kwa wale wanawake wanaelewa,na pia
alikuwa hana muda ama kipindi maalum cha kuingia katika hedhi muda wowote
alikuwa anaweza kuingia na kupata maumivu makali sana.
Baadhi ya wanafunzi ambao pia wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo hilo wakiwa katika semina hiyo iliyoandaliwa na mrembo MILLEN MAGESE wikiend hii jijini dar es salaam |
MILLEN MAGESE anapokumbuka mateso aliyopitia haachi kulia hata mbele za watu kwa inauma sana,katika semina hii alimwaga chozi |
Tatizo hilo lilimsumbua kwa takribani miaka yote
ambayo aliyokuwa nchini na madaktari nchini walishindwa kujua nini hasa
kunamsumbua.MILLEN baada ya kwenda kuishi Africa ya kusini tatizo hilo lilizidi
sana na kuamua kuwaona wataalam mbalimbali nchini humo kwa ajili ya vipimo ambapo walifanikiwa kujua ni tatizo gani
lilimpata.
ENDOMETRIOSISI ni ugonjwa ambapo ni mgeni sana
masikioni mwa watanzania ambapo hata kishwahili chake bado hakijapatikana ni
ugonjwa ambao humsababishia mgonjwa maumivu makali sana kipindi cha hedhi na
husababisha pia mgonjwa kutopata mtoto.
Huu ndio ugonjwa uliomkuta mrembo MILLEN MAGESE
ambapo ilibidi afanyiwe upasuaji wa kizazi kwa mara 12 nchini Africa ya kusini
kwa ajili ya kutibu ugonjwa huo jambo ambalo linasikitisha sana.
akitoa semina |
“Nimefanyiwa upasuaji wa kizazi mara 12 nchini Africa
ya kusini kwa msaada wa marafiki zangu ili kuokoa maisha yangu,sina uwezo wa
kupata mtoto tena mirija yangu yote imeziba na madactari wanasema haiwezi
kuzibuka tena”aliiambia habari24.
Mrembo huyo kwa sasa yupo nchini na HABARI24 BLOG
imefanikiwa kukutana naye na kufanya naye mahojiano maalum ambapo ametueleza
lengo lake la kurudi nchini Tanzania
“Nimekuja Tanzania sasa kwa lengo moja kuwaokoa
watanzania na kuwajengea uelewa juu ya ugonjwa huu chini ya mpango wangu wa MILLEN MAGESE
FOUNDATION ,kwa sababau ugonjwa huu kwa hapa Tanzania unaonekana bado
haufahamiki japo watu wengi sana unawasumbua kiasi kwamba wanakosa raha
maishani na kikubwa zaidi hakuna hata kipimo cha ugonjwa huo hapa nchini Tanzania”aliiambia
HABARI24 BLOG
Kwa kuanza na hilo la kuwaelimisha watanzania
wikiend hii mtandao huu ulimshughudia mrembo MILLEN akiwa anatoa semina kwa
wanafunzi,kina mama na watanzania zaidi ya mia moja juu ya ugonjwa huu ambapo walimshukuru
sana kwa huduma hii.
Katika maongezi yake MILLEN ameigeukia serikali na
kuiomba kuhakikisha unawasaidia wagonjwa wa ENDOMETRIOSIS ikiwa ni pamoja na
kuwajengea hospitali maalum ya ugonjwa huo
USIKOSE HAPA HAPA TUTAKUPA USIKIE SAUTI YAKE AKIZUNGUMZA NASI
No comments:
Post a Comment