Wednesday, June 4, 2014

TIGO,AIRTEL NA ZANTEL SASA WAUNGANA,WATANGAZA KUSHIRIKIANA KATIKA HUDUMA ZA KUTUMA NA KUPOKEA PESA.TUKIO NZIMA LA MUDA MCHACHE ULIOPITA LIKO HAPA

Mkurugenzi mkuu wa tigo tanzania DIEGO GUTIEREZ akizungumza na wanahabari mapema leo kuhusu ushirikiano huo
          Kampuni za mawasiliano Tanzania za TIGO,AIRTEL,NA ZANTEL leo wametangaza kuingia katika ushirikiano wa pamoja utakaowezesha wateja wao wa tigo pesa,airtel money,na ezy pesa kutumiana  fedha kupitia simu zao za mkononi,huduma ambayo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi juni.
Huu ni ushirikiano wa kwanza na wa aina yake barani Africa inayowezesha wateja wa kampuni tofauti za simu kuwa na uwezowa kutumiana na kupokea fedha moja kwa moja kwenye account zao za simu tofauti na ilivyokuwa hapo awali.
Mkurugenzi wa zantel PRATAP GHOSE akifafanua jambo akiwa na mkurugenzi wa tigo DIEGO GURIEREZ, pamoja na mkurugenzi wa airtel tanzania  SUNIL COLASO
 Kupitia huduma hii wateja wa kampuni hizi tatu watakuwa na uwezo wa kutuma pesa kutumia simu zao za mkononi moja kwa moja kwa mujibu wa taarifa ya pamoja kutoka kwa makampuni hayo.
Huduma hiyo leo imezinduliwa rasmi mbele ya wanahabari na mameneja wa makampumpuni yote matatu ambapo akizungumza mbele ya wananahabari mkurugenzi mkuu  wa tigo DIEGO GUTIEREZ amesema kuwa kampuni ya tigo wanafurahi sana kushirikiana na makampuni hayo kwa ajili ya kuendeleza huduma ya kutuma na kupokea pesa nchini Tanzania na kaongeza kuwa tigo inawahakikishia wateja wote kuwa huduma hiyo ni salama kabisa kwa matumizi ya kutuma na kupokea fedha.
Kwa upande wake mkurugenzi wa airtel bw SUNIL COLASO amesema kuwa airel imejikita katika kuwapa wateja wake huduma zenye ubunifu wa hali ya juu bila kujali ushindani wa kibiashara lengo kuu likiwa ni kuwapa wateja wake nchi nzima fursa na uweo wa kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao.
Aidha mkurugenzi wa zantel PRATAP GHOSE amesema zantel inadhamira ya dhati  kuhakikisha thamani na ubunifu wa huduma zake ,na ni kwa sababu hiyo kampuni ya zantel imefurahia ushirikiano huo ambao utawasaidia wateja wake kufanya biashara zao kwa urahisi zaidi.   

No comments: