Wednesday, June 4, 2014

HAWA NDIO VIJANA WAWILI WA COPA COCA COLA WALIOPATA NAFASI YA KWENDA BRAZIL KUPATA MAFUNZO YA SOKA NA KUCHEKI MECHI YA UFUNGUZI WA KOMBE LA DUNIA

 Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda akizungumza na wanahabari katika makabidhiano hayo 
 Wachezaji wawili waliochaguliwa kwenda kwenye kambi ya Copa Coca-Cola ya Dunia nchini Brazil wamekabidhiwa bendera tayari kwa safari hiyo inayofanyika leo (Juni 4 mwaka huu).

Hafla ya kukabidhi bendera hiyo kwa Ali Shabani Mabuyu na Juma Yusuf imefanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juliana Yassoda ndiye alikabidhi bendera.
Wakikabidhiwa bendera
 Wakati Mabuyu kutoka Ilala alikuwa mchezaji bora wa michuano ya Copa Coca-Cola kwa vijana wenye umri chini ya miaka 15 kwa mwaka 2013/2014, Yusuf kutoka Zanzibar ndiye aliyeibuka mfungaji bora katika michuano hiyo.

 Vijana wawili ambao ni  Ali Shabani Mabuyu na Juma Yusuf wakiwa ndani ya bendera ya tanzania
Wachezaji hao watakuwa katika kambi hiyo itakayokuwa katika Jiji la Sao Paulo kwa siku kumi ambapo watafundishwa masuala mbalimbali ya mpira wa miguu. Pia watashuhudia mechi ya ufunguzi ya Fainali za Kombe la Dunia katika ya wenyeji Brazil na Croatia itakayochezwa Juni 12 mwaka huu.

No comments: