Saturday, June 21, 2014

USAFIRISHAJI WA FEDHA KIHOLELA NI HATARI---WATANZANIA TUMSIKILIZE KAMISHNA KOVA

      
Pamoja na  jitihada kubwa zinazofanywa na jeshi la
polisi kanda maalum dar es salaam pamoja na Tanzania kwa ujumla katika kupambana
na uhalifu wa aina mbalimbali katika jiji letu la dar es salaam,jitihada hizo
haziwezi kuzaa matunda mema kama watanzania wenyewe hatutahakikisha
tunashirikiana na jeshi la polisi katika kufichua uhalifu wa
aina yoyote uliopo katika mitaa yetu.
          
       Wahalifu
ni watu ambao wamekuwa wakitumia muda wao wote kubuni na kuhakikisha wanakuwa
na mbinu mpya katika kufanya uhalifu wao jambo ambalo limekuwa likigfanya
vyombo vya usalama kufanya kazi usiku na mchana ili tu kupambana na uhalifu wa
aina yoyote hapa nchini.
       
      Ushafirishaji
wa fedha kiholela katika jiji la dare s salaam ni jambo ambalo limekuwa
likisababisha uhalifu mkubwa sana katika mitaa yetu ikiwa ni pamoja na wahalifu
kufanya uvamizi katika magari ambayo yanasafirisha fedha hizo,na hatimaye
kuzipora jambo ambalo mwisho wa siku lawama zinaliendelea jeshi la polisi moja
kwa moja bila kutambua kuwa kuna uzembe wa wasafirishaji.
       
      Matukio
hayo sio mageni tena masikioni mwetu hasa miaka hii ya karibuni kwani kila
mwezi lazima usikie aidha tukio moja la gari lililovamiwa njiani na kupora
mamilion ya fedha na baadaye wahusika husema walikuwa wanapeleka hela benk,au
walikuwa wanatoa benk kwende kulipa mishahara mbalimbali.
        
      Tunapozungumzia usafirishaji wa fedha
kiholela tunazungumzia pia Kubeba fedha kiholela katika mifuko ya plastiki
maarufu kama  “RAMBO” au mifuko mingine.Kubeba
fedha katika pikipiki ndani ya mfuko unaobebwa mgongoni.Kusafirisha fedha hizo
ndani ya magari bila tahadhari yoyote.Kukusanya fedha za kibiashara katika
vituo mbalimbali vya mauzo bila utaratibu maalum au kusindikizwa na walinzi Kuhifadhi
fedha nyingi ndani ya nyumba au katika ofisi mbalimbali, n.k
       
    
 Kamishna
wa polisi kanda maalum ya dar es salaam SULEMAN KOVA ni moja kati ya watu ambao
amekuwa akitumia muda wake mwingi sana kulizungumzia swala hili la usafirishaji
wa fedha kiholela na kutaja madhara yake kila akutanapo na vyombo vya habari
lakini watanzania bado tumekuwa hatumwelewi.
         
      Kamishna
KOVA amekuwa akinukuliwa na wanahabari akiwasihi watanzania kuomba ulinzi wa
jeshi la polisi pindi wanapotaka kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha kutoka
sehemu moja kwenda nyingine na akisisitiza kuwa jeshi la polisi lipo kwa ajili
ya watanzania na lipo tayari kufanya kazi hiyo pindi wewe msafirishaji wa fedha
unapoomba msaada wa jeshi hilo.
       
     Kwa kutambua
madhara makubwa ya kusafirisha fedha nyingi kiholele kama kuvamiwa,kuporwa,na
hata kuuawa na wahalifu hao pia anatumia muda wake kuwaeleza watanzania njia
nyingine ambazo unaweza kuzitumia kutoa fedha sehemu moja hadi nyingine ikiwa
ni njia za mitandao ya simu kama M-PESA,TIGO PESA,AIRTEL MONEY  na nyingine nyingi ambazo zipo hapa nchini
kwa sasa.
        
     Aidha
kamishna KOVA anawataka wadau wote wa kusafirisha fedha  kuwa  wawe na account za fedha ili kuwa na uwezekano
wa kutumia cheque, kadi za ATM, kufanya miamara bila kadi (Cardless
Transaction) kwa njia ya mtandao. 
     
       Njia hizi za mitandao ya simu ni moja kati
ya njia rahisi na salama za kusafirisha pesa badala ya kutembea na kiasi
kikubwa cha fedha ambacho kinaweza kusababisha madhara kwa msafirishaji kwani
mhalifu ni mtu ambaye halali.
             
      Tukumbuke kuwa Wahalifu wanazo taarifa
za kutosha na pia wana mawasiliano ya kutosha na watu mbalimbali wa karibu na
watu wote wanaotajwa. Wahalifu wana mawasilianoo na baadhi ya madereva, baadhi
ya wahasibu, baadhi ya watumishi wa ndani, pamoja na ndugu na jamaa wa karibu
na watu wenye kujihusisha na biashara au namna nyingine yeyote inayomfanya mtu
asafirishe fedha au kuzitunza kama ilivyotajwa hapo juu. 
          
       Ni jukumu la kila anayehusika
kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuacha mitindo yenye ushawishi kwa
wahalifu.
Mtandao
huu unachukua nafasi hii kuwasihi watanzania wote ambao wamekuwa wakisafirisha
fedha hizi bila kuwa makini kuwa tulisaidie jeshi la polisi kwa kuwa makini
pindi tunapofanya hivi badala ya kufanya uzembe huu na baadae kulitupia lawama
jeshi letu la polisi.


No comments: