Wednesday, June 4, 2014

WIKI YA MAZINGIRA YAINGIA SIKU YA TATU,WAZIRI MAHENGE ATEMBELEA KIWANDA CHA BIA TBL MWANZA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Dk. Eng. Binilithi Satano Mahenge wa pili (kulia), akiwa katika ziara yake ya kukagua mazingira ya Kiwanda cha bia (TBL) kilichopo kata ya Pasiasi wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, na wa pili (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete,wakati maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yakiendelea jijini Mwanza.


Mh. waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais -Mazingira,Dk. Eng. Binilithi Satano Mahenge wa kwanza (kulia), Naibu Waziri Mh. Ummy Mwalimu wa kwanza (kushoto)na Mkuu wa Mkoa Eng. Everist Ndikilo wa pili (kulia) wakizungumza na mmiliki wa Kiwanda cha Coca Cola (Nyanza bottling) Bw. Christopher Mwita Chuma baada ya kuwasili ofisini kwake leo jijini Mwanza.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mh. Ummy Mwalimu wa kwanza (kushoto)akiwa anafanya usafi eneo la mtaa wa Pamba A jijini Mwanza stendi ya zamani.

No comments: