Mwenyekiti wa Bongo muvi akitoa hotuba ya kuuaga mwili wa marehemu kwa wasani pamoja na wananchi waliohudhuria. |
Mwili wa aliyekuwa mtayarishaji wa filamu Marehemu George Otieno Okomu unaagwa muda huu katika viwanja vya Leaders jijini Dares salaam.
Wasanii pamoja na wananchi wamejitokeza kwa wingi kumuaga msanii mwenzao mwenye asili ya Kenya ambaye amefanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya Filamu hapa chini. Marehemu George alifariki kwa ajali ya gari siku ya ijumaa akitokea Dodoma. Mwili wa msanii huyo utapelekwa viwanja vya ndege vya Mwalimu Nyerere ambapo utafirishwa kesho kwenda kwao Kenya kwa ajili ya taratibu za mazishi.
No comments:
Post a Comment