Thursday, July 31, 2014

MAGAZETI YA LEO IJUMAA

1_f60b6.jpg


2_be4be.jpg
3_676cf.jpg

MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM

1a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika  Kusini na Festus Mogae wa Botswana wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa Africa Readership Forum ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia changamoto hizo.
2a
Rais mstaafu wa wa Afrika  Kusini Thabo Mbeki  akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
3a
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika  Kusini katikati ,Festus Mogae wa Botswana kushoto na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa wakiwa wakiongoza mkutano huo.

HALI YA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA BADO TETE,LHRC WATOA REPORT YAO YA NUSU MWAKA,JIONEE HAPA

Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za Binadamu Bi HELLEN KIJO BISIMBA akizungumza na waaandishi wa habari mapema leo kuhusu Repoti hiyo
          Kituo cha sheria na haki za binadamu tanzania LHRC leo kimetoa report yake ya nusu mwaka ya haki za binadamu report ambayo inaonyesha  bado hali ya haki za binadamu kwa Tanzania ni tete na jitihada za serikali bado zinahitajika kujinasua na hali hiyo.
         
       Katika repoti  hiyo ya miezi sita tu inaonyesha kuwa watu 320 wameuawa kwa imani  za kishirikina ukilinganisha na watu 303 waliouawa mwaka jana pamoja na  matukio 473 yameripotiwa kuuawa kwa watu na wananchi wanaojiita wenye hasira kali ukilinganisha na matukio 597 ya mwaka jana ambapo takwimu inaonyesha kupungua,
Mwanasheria kutoka LHRC,  MLOWE  akifafanua yaliyomo ndani ya  Report hiyo
Aidha report hiyo inaonyesha matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yameanza kuongezaka kwa kipindi cha miezi sita iliyopita ambapo watu wawili wameripotiwa kuuawa na wengine kujeruhiwa vibaya.
           
Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es salaam mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho bi HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa maswala mengi kama mauaji ya vikongwe,mauaji ya walemavu wa ngozi,migogoro ya ardhi,ajali za barabarani,wananchi kujichukulia sheria mkononi,na mambo mengine kama hayo bado ni changamoto kubwa kwa nchi ya tanzania ambapo amesema ni lazima serikali akazie mkazo maswala hayo.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini
Bi HELLEN amesema kuwa ili kudhibiti hali hii ni lazima kwa elimu ya haki za binadamu irudishwe kwenye mfumo wa elimu rasmi wanchi,pamoja na serikali kutunga sheria inayolinda haki za mtoa taarifa ili kuweza kupata ushirikiano wa wananchi katika mapano dhidi ya vitendo viovu.

     Aidha ameitaka serikali kuboresha mifumo ya utoaji haki ikiwa ni pamoja na mahakama na mabaraza mbalimbali ya utatuzi wa migogoro ili kukuza dhana ya utawala wa kisheria nchini
Report hiyo imetoka leo ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya wanawake wa Africa inayoadhimishwa kote Africa.

Wednesday, July 30, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMIC JULAI 31,2014,HABARI,MICHEZO NA BURUDANI.USIKOSE

1_7d8ae.jpg
2_fc8c2.jpg
3_9c34f.jpg

USIKOSE TAMKO HILI ZITTO LA EDWARD LOWASA KUHUSU KUHUSISHWA NA ACT

Katika gazeti la Tanzania Daima toleo na. 3536 la tarehe 30 Julai, kuna habari inayosema Lowassa aibukia ACT na kumuhusisha na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) Zitto Kabwe katika kile gazeti hilo kilichodai mikakati ya siri dhidi ya Chadema.

Habari hizo ni uzushi, na ni muendelezo wa mikakati ya kumchafua na kumgonganisha Mh Lowassa na wanasiasa wenzake wa kada na maeneo mbalimbali.

siasa na maajabu yake--TAZAMA HAPA TUKIO LA AINA YAKE SHINYANGA,MADIWANI WA CHADEMA WALIOHAMIA CCM,WARUDI CHADEMA TENA

Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Hali ilikuwa tete,ngumi zikanukia-kulia ni mmoja wa viongozi wa chadema katika manispaa ya Shinyanga akikabiliana na wanachama wa chadema waliotaka kuleta vurugu uwanjani hapo



Wananchi wakiwa na Hasira kuona madiwani waliowaita wasaliti wakirudi chadema tena_Hapa ni katika viwaja vya mahakama ya Mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga ambako  kumefanyika mkutano wa aina yake ambao pengine unaweza kuuita mkutano wa kihistoria,mkutano ambao uliandaliwa na viongozi wa CHADEMA kanda ya ziwa mashariki wakiongozwa na mbunge wa Maswa mashariki Sylivester Kasulumbayi.Katika mkutano huo wale madiwani wa Chadema ambao mwezi Februari mwaka huu,walijiuzulu na kuhamia CCM,Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo na Sebastian Peter kata ya Ngokolo,leo wameomba radhi na kurudi CHADEMA. Walisema waliahidiwa na viongozi wa juu wa ccm akiwemo Nape Nauye,Mwigulu Nchemba,Ridhiwani Kikwete,Steven Masele n.k kuwa wahame Chadema waende CCM ili baadaye wajiunge na ACT ili waiimarishe lakini wameshindwa kutofautisha ccm na ACT hivyo kuamua kurudi chadema kwani ndiyo chama imara.Walisema waliambia huwezi kuwa ACT ucpitie CCM.Ikumbukwe kuwa madiwani hao walihamia CCM kwa mbwembwe nyingi wakidai CHADEMA haifai kinaendekeza ubinafsi,ukabila n.k,ikafikia hatua wakaitwamadiwani mizigo.

Waliletwa na pikipiki kwenye mkutano_Aliyevaa nguo ya kijani(CCM) ni bwana Zacharia Mfuko diwani wa CHADEMA kata ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga baada ya kuwasili katika mkutano wa Chadema leo jioni,baadaye alivua nguo hizo na kuomba radhi kuwa alikosea njia baada ya kushawishiwa na viongozi wa CCM akiwemo Stephen Masele,Nape Nauye, Habib Machange na viongozi wengine wengi ndani na nje ya chadema na CCM,na kueleza kuwa ccm hawana lolote badala ya kulaghai watu kwa kutumia pesa.

Kijani peke yao_Kulia ni Sebastian Peter diwani wa Ngokolo akiwasili katika eneo la mkutano,leo.Katika hali ya kushangaza baada ya madiwani hao kuwasili kwenye mkutano vurugu za hapa na pale zilitawala takribani dakika 15 lakini baadaye hali ilikuwa shwari baada ya mbunge Kasulumbayi kutoka jimbo la Maswa mashariki kutumia akili na nguvu nyingi kutuliza wanachama wa Chadema waliokuwa na hasira na kutopendezwa na kitendo cha kuwaleta wasaliti wa chama eneo hilo

 Madiwani wasaliti kama wanavyoitwa   hivi sasa hapa Shinyanga,wakiwa na nguo za CCM wakiwa wamekaa na viongozi wa CHADEMA baada ya kuwasili eneo la mkutano jioni ya leo.

Mkutano huo ni wa aina yake umehudhuriwa na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga,kila mtu akiwa na lake moyoni,wengine wakisema CHADEMA wawapige chini madiwani hao,wengine wakisema wasamehewe kwani mungu karudisha kondoo wake waliopotea.

Diwani Sebastian Peter kulia akinong'ona jambo na mbunge Kasulumbayi.

Wengine walilia kwa hasira_Wananchi wakiwa hawaamini kilichokuwa kinaendelea uwanjani hapo,matusi yalitawala.Picha na Kadama 

Ilikuwa siyo hali ya kawaida-wengi walibaki midomo wazi,walipigwa na hali ya mshangao,wenye kushika viuno haya,wenye kununa haya,wenye kutukana haya,wenye kusema bora liende nao walikuwepo,wenye kuisikitikia chadema kwa kupokea watu wanafiki na wasaliti haya,wenye kukumbuka mbwembwe za CCM wakati wa kuwanyakua madiwani hao wa chadema tena katika eneo hill hilo nao hawakukosekana.

Madiwani hao wawili wakiwa jukwaani tayari kuzungumza na wananchi wa Shinyanga,kulia ni mbunge Kasulumbayi akiwakaribisha.

Tunavua uccm-Kama walivyovua magwanda ya CHADEMA mbele ya Nape Nauye wa CCM,leo madiwani hao wamevua pia nguo za CCM,lakini tofauti na kipndi kile leo hawakuchoma moto nguo.

HABARI NZITO LEO--BAADA YA LOWASA KUTAJWA KUKIFADHILI CHAMA KIPYA CHA ACT,DK SLAA AIBUKA,ASEMA MAZITO,SOMA MTIRIRIKO MZIMA HAPA


  

Na Karoli Vinsent

     SIKU moja kupita Baada ya Gazeti la Tanzania Daima kufichua kile ilichokiita ni hujuma mbaya ya Kisiasa anayoifanya Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) kwa kushirikiana na  wanachama waliofukuzwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa usaliti kwenye chama hicho.

             
      Wanachama hao ambao wamejiunga na Chama kipya cha kisiasa cha Allaince for Change and Transparency (ACT-Tanzania)  chama ambacho inasemekana kinaubia na Chama kikuu nchini kwa lengo la kukiboma Chadema.


              
      Naye Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dk Wilbroad Slaa,ameibuka na Kumvaa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM na kusema  Chadema hakina mda wa kupoteza na kupambana mtu mwenye Tamaa ya Urais huku akijua hana sifa kushika nafasi hiyo. 


      Kauli hiyo kali Imetolewa Mda huu na Katibu huyo Mkuu wa Chadema Dk Wilbroad Slaa wakati alipokuwa anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu kwa njia ya Simu kuhusu taarifa iliyoandikwa kwenye Gazeti hilo la kila siku kuhusu mipango hiyo michafu ya kisiasa.

             
       Ambapo alisema Taarifa hizo amezisikia na kusema chadema hakina mda mchafu wa kumfikilia mtu anayetafuta nafasi ya Urais huku akijua hana sifa.
                
    “Ngoja nikwambie Chadema imejipanga kuhakisha tunafika mbali kisiasa na hatuna mda mchafu wa kupambana na mtu anayesaka Urais huku hakijua hana sifa, kwanza haya ni Maajabu mimi najua  vyama vinazaliwa ili kupambana na chama kilichopo madarakani ambacho kimeshindwa kuondoa umasikini kwa mda wa miaka 50 nashangaa leo hiko chama cha ACT kinaungana ili kupambana na chama cha upinzani?”Alihoji Dk Slaa


             

      Dk Slaa ambaye chama chake ndicho chama kikuu cha upinzani Nchini ambacho kinaanza kufanyiwa Hujuma, alikitabilia mwisho Mbaya chama hicho  kipya cha kisiasa cha  Allaince for Change and Transparency (ACT-Tanzania)  na kusema kama kimeanzisha na Mamluki ili kije kupambana na Upinzania hapa nchini Basi hakitafika mbali na kufuata nyayo ya vyama vilivyokuwa huku nyuma.
           
        Katika Hatua nyingine Dk Slaa,alisema kwa sasa wamebaini kuna Mamluki wameanza kupenyeshwa ndani ya Chadema kuelekea uchaguzi wa ndani wa chama cha CHADEMA.
             

Tuesday, July 29, 2014

MAGAZETI LEO EID PILI JUMATANO JULY 30,2014

3_f7042.jpg
4_47118.jpg

HUZUNI KUBWA--HALI YA MSANII BAHATI BUKUKU SIO NZURI,MAOMBI YAHITAJIKA KUOKOA MAISHA YAKE


                                                     Na Karoli Vinsent

HALI ya Msanii Hodari wa Nyimbo za Injili Nchini Tanzania Bahati Bukuku inazidi kuwa mbaya,sasa kinachoitajika ni Maombi na sala  kutoka kwa Watanzania ndio itakayoweza kumwokoa Msanii huyo wa Injili,Mtadano umeambiwa.
       
  Bahati Bukuku,ambaye alipata ajali mbaya ya Gari iliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili  iliyopita kwenye eneo la Ranchi ya Narco wilayani Kongwa  Mkoani Dodoma m,ajira ya saa tisa usiku wakati alipokuwa anakwenda Mkoani Shinyanga,Kahama kwenye mkutano wa Injili ambapo ajali ndiyo iliomleta matatizo makubwa.
          
  Akizungumza na Mwandishi wa Mtandao kwa Njia  ya Simu Rafiki wa karibu wa bahati Bukuku,ambaye akutaka kutaja Jina kwenye Mtandao huu kwa kusema yeye sio msemaji wa Familiya Bukuku alisema kwa sasa hali ya Bahati bukuku inazidi kuwa mbaya sana na  sasa kinachoitajika ni sala na Maombi tu.

      “Da leo nimeoka kumwangalia Hospitali yaani da hali ya Rafiki yangu Bahati Bukuku ni mbaya sana na kinachoitajika sahivi ni maombi tu,maana ukimwangalia mpaka unapatwa na huruma sana tena unapata maswali ya kujiuliza huyo ndio msanii mwenye afya tele juzi tu?”alihoji mpashaji huyo Habari

RAIS KIKWETE ASALI SWALA YA IDDI DAR ES SALAAAM

D92A2961
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
D92A2982
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kuswali sala ya Iddi El Fitr katika mshikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
D92A3004
D92A2839
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakiswali sala ya Iddi El Fitr katika masjid Maamur Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

BARAZA LA EID LAFANA ZANZIBAR

IMG_8612
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake kwa Wananchi na Waislamu katika Baraza la Eid El Fitri lililofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
IMG_8557
Baadhi ya Viongozi na wageni mbali waliohudhuria katika sherehe za Baraza la Eid el Fitri wakiangalia na kusikiliza Hotuba iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katikaukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.] IMG_8632
Baadhi ya Wananchi na Waislamu wasikiliza hotuba iliyotolewa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja,katika kusherehekea Sikukuu yaEid el Fitri,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.] IMG_8694
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwaongoza wake mbali ,mbali wa Viongozi wa Kitaifa pamoja na wananchi  waliohudhuria katika sherehe za Baraza la Eid el Fitri wakielekea   kupata viburudishaji baada ya kumalizika kwa Hotuba   iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein  katika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Unguja leo. [Picha na Ramadhan OthmanIMG_8822
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na wake wa Viongozi (pichani) akipena mkono na Mama Fatma Karume,(kulia) akiwepo na Mama Mwanamwema Shein katika viwanja vya ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Zanzibar,(wa pili kushoto) Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.