Thursday, July 10, 2014

EXCLUSIVE--WAZIRI NYALANDU AIBUKA NA KAULI NZITO JUU YA MAGAZETI YANAYOMCHAFUA,AKIRI KUMUUNGA MKONO MEMBE MBIO ZA URAIS.SOMA HAPA



NA KAROL VICENT

               BAADA ya kuandikwa sana kwenye Vyombo mbalimbali vya Habari nchini,Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu,ameibuka na kusema yote mabaya yanayozungumziwa anamwachia mungu,kwani wananchi wanamfuhamu kwa kazi nzuri anayofanya.
       
        Kauli hiyo ametoa Usiku wa kuamkia leo Jijini Dar Es Salaam kwenye Hoteli ya Kimataifa ya Hyatt Regency,wakati alipokuwa anafanyiwa Mahojiano na Mwandishi wa Mtandao huu,ambapo mwandishi wa Mtandao huu alipotaka kufahamu ukweli unaoandikwa kwenye Magazeti mbalimbali kuhusu yeye,ndipo waziri Nyalandu alisema anamwachia wananchi kwani kinachaondikwa hakina ukweli wowote.


        “Sikiliza mwandishi nimeandikwa sana vibaya na Magazeti tena wengine wakinitaja kabisa kwamba mimi ni Jangili kama vile wanaushahidi ,baada ya kuniona niko kimya wengine wakasema mimi ni Jasus wa CIA,ambaye nimepandikizwa kwenye utawala huu mimi namwachia mungu tu kwani habari wanazoandika ni za uongo hazina ukweli kabisa”alisema Nyalandu.

      Nyalandu,aliyataja magazeti ambayo yanamwandika Vibaya , magazeti hayo ni Jamhuri gazeti,Fahamu,Dira Mtanzania,Raia Mwema,magazeti hayo ambayo yanatoka maramoja kwa Wiki.mwandishi wa Mtandao huu alipomuuliza kwanini asiyachukulie Hatua kile wanachoakiandika kama ni cha Ukweli au la?

       Nyalandu,alisema kwasasa hawezi kuyachukulia hatua yeye anachokufanya ni kuongeza ujuzi wa Ufanyaji kazi kwenye Wizara hiyo,na wanaotaka kuendelea kumwandika vibaya wamwandike tu kwani wananchi wanaujua mchango wake kwenye Wizara hiyo.

      Kuhusu ukweli wa Taarifa ya kwamba ni Jasus wa CIA
Waziri Nyalandu alisema hakuna hata ukweli wowote kwamba yeye ni Jasus kwani ,hata hafamiani na hao majajus na kwanza ni hivo ni vichekesho.

        “Hivi kweli leo Naungana na Mh Ridhiwani Kikwete kwamba waandishi wengi wa Nchi hii ni Makanjanja kwamba hakuna ukweli wowote kwanza hawajuai wanavyoandika hivyo wanamwaibisha Rais wetu wa Nchi kwani sisi tunavyochaguliwa tunakuwa tumefuzu sehemu zote na tunakuwa hatuna Kashfa yeyote ndio maana Rais anatuamini”alisema Nyalandu.

      Kuhusu kuhusika kumpigia Kampeni Waziri Membe kwenye nafasi ya urais 2015 kwa madai ya kuadiwa kupewa Uwaziri Mkuu.
Waziri Nyalandu ambaye ni Waziri Kijana alizidi kusema taarifa hizo ni za ukweli,kwani Waziri Membe ni Rafiki yake lazima atakuwa Rais 2015.

        “Ndio mwandishi lazima nimpigie Kampeni membe anafaa kuwa Rais na mwakani lazima aingie ikulu,na hapa ninavyongea na wewe nikimaliza hapa kuongea na wewe naenda kuongea nae waziri membe nakuhakishia lazima awe Rais 2015,kwani anasifa zote kwani wewe mwandishi huoni sifa alizokuwa nazo?unamfananisha na wengine hao”alizidi kusema Nyalandu.

       Kuhusu Waziri Nyalandu na Waziri kivuli wa Wizara hiyo Mchungaji Piter Msigwa kuipigia chapuo kampuni ya Uwindaji ya Windrose Safari(WWS) inayomilikiwa na wamarekani huku haina Sifa.

      Waziri huyo ambaye alionekana kujibu maswali kwa Hasira alisema Wizara yake haifanyi kazi kimajungu.

       “Hizo taarifa zinaandikwa sana kwenye Magazeti hazina ukweli wowote.kwanza mpaka unapewa kibali kwenye Kampuni ya Uwindaji lazima uwe na Vigezo vyote kampuni hii inayo ndio maana tumeipa nafasi hiyo sasa hao wanaolalamika huko kwenye Magazeti fahamu kwamba hawana sifa hata kama kampuni yao ni ya Mzawa”alisidi kusema nyalandu.

      Kuhusu DVD aliyoitoa Waziri Kivuli wa Wizara hiyo mchungaji Piter Msigwa.

          Nyalandu alisema taarifa hizo amezipata na ameunda tume kuichunguza huo mkanda na kujua kwamba taarifa hizo ni za kweli,.
“Nimeunda tume kuchunguza ukweli wa huo mkanda na nimewapa wiki mbili na waje na majibu ya kulidhisha ili tubaini ukweli wa ushahidi huo anausema msigwa na kwamba ni ukweli au la basi hatua zichukuliwe “alisema Nyalandu.

No comments: