Wednesday, July 9, 2014

MSAADA--TAASISI YA WATOTO YATIMA YA BABU SAALAM WANAOMBA MSAADA WAKO WA HALI NA MALI

MWENYEKITI  wa taasisi ya Babu Saalam Tabazati iliyopo Magomeni Mapipa Jijijni Dar e Salaam Sheikhe Alhaji Msii 
       MWENYEKITI  wa taasisi ya Babu Saalam Tabazati iliyopo Magomeni Mapipa Jijijni Dar e Salaam Sheikhe Alhaji Msii ameitaka jamii kuwasaidia watoto yatima wanaolelewa na Taasisi yake kwa kushirikiana na zawiya  Kadiriya iliypo Kariakoo jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na HABARI24 BLOG Jijini Dar es salaam  Alhaji Msii amesema watoto hao ambao wametoka maeneo mbalimbli katika mikoa ya Tanzania wanalelewa na kusomeshwa elimu ya Dini ya Kislaam huku wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kibinadam.
Alhaji Msii alizitaja changamoto hizo malaz,chakula pamoja na mavazi amesema wengi wawototo hao wanatokea mikoa ya Kondoa,manyara na Singida amesema watoto hao ambao kwa sasa wana Soma katika zawiya hiyo ambayo kwa sasa ipo chini ya  Sheikhe Khamisi Kifulu baada ya mwasisi wa zawiya hiyo  Sheikhe Khalifa Ramiya kufalili dunia

Kwayeyote atakaetaka kuwasaidia watoto hawa awasaidie kwa simu namba 0786124878 
Baadhi ya watoto ambao wanalelewa katika Taasisi hiyo cha Babu Saalam Tabazati kilichopo magomeni jijini dar es salaam ambao wanahitaji msaada wako wa hali na mali wewe kama Mtanzania

No comments: