JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam limewatoa Hofu wakazi wa Jiji hili,na kusema viungo vya binaadamu
vilivyogundulika katika maeneo ya Mbweni Mpiji ni Vimetoka kwenye Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba
na Teknolojia (International Medical and Technological University –IMTU,ambapo vilikuwa vikitumika katika kujifunzia
na sio Maeneo mengine.
Hofu imetolewa leo na
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleman Kova wakati wa
Mkutano na waandishi wa Habari ambapo Alisema kuwa, Jeshi la polisi
lilipokea taarifa 21 Julai mwaka huu, majira ya jioni kutoa kwa wasamaria wema
na ndipo jopo la wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Kipolisi
Kinondoni ACP Camilius Wambura kufika maeneo hayo majira ya jioni.
“Katika hatua za awali baada ya kufika
eneo la tukio waligundua mifuko 85 meusi yenye viungo vya aina mbalimbali vya
binaadamu kama vile Vichwa, Miguu, Mikono, Mioyo, Mapafu, Vifua na Mifupa ya
aina mbalimbali ya binaadamu”
Alieleza kuwa, katika hali iliyoshangaza
kuwa viungo hivyo havikuwa na uvundo wala haraufu ya aina yoyote na vilionekana
kwamba vimekaushwa na kukakamaa.
“Katika eneo hilo pia vilikutwa vifaa
vinavyotumikaa hospitalini kama vile mipira ya kuvaa mikononi (gloves) mifuko
miwili iliyotumika, nguo maalum (apron) zipatazo 20 na karatasi mbili zenye
maswali ya kujibu”
Alisema kuwa licha ya eneo la tukio
kuwepo wananchi waasiopungua 1000 lakini hakuna aliyekuwa na taarifa
saahihi juu yaa sakata hilo.
“Viungo viliweza kuchukuliwa
na kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kufanyiwa uchunguzi,
chini ya Jopo la Wapelelezi likiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Kanda ya Maalum
ACP Japhari Mohamed akisaidiana na Daktari wa Jeshi la Polisi anayehusika na
miili ya binaadamu” alisema.
Kamishna Kova alieleza kwamba, baada
ya uchunguzi wa kina kufanyika ilibainika kwamba viungo hivyo kwa mara ya
mwisho vilikuwa katika Maabara ya IMTU jijini Dar es Salaam.
Katika hali nyingine isiyokuwa ya
kawaida Kamishna Kova alisema, wananchi wa eneo hilo waliopata taarifa waliamua
kulishikilia gari ndogo aina ya Canter ambalo lilikuwa limebebaa uchafu
uliokuwa unatoa harufu kali na kulihisi kuwa limebeba mifuko mingine ilkiyokuwa
na miili ya binaadamu.
“Gari hilo lilibainika wazi kwamba
halikuhusika na tukio hilo, pia tulipolipekewa ikagundulika limebeba mabaki ya
kuku ikiwemo Utumbo, miguu, vichwa na manyoya pamoja na uchafu mwingine
uliokuwa umeoza” alisema.
Katika kuhakikisha unapatikana
ushahidi wa kina Kamishna Kova alibahinisha kuwa Jeshi la Polisi litamuhusisha
Mkemia Mkuu wa Serikali na baada ya kukamilika kwa uchunguzi jalaada
litaapelekwa kwa Mwaanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zake ili sheria
ichukue mkondo wake.
No comments:
Post a Comment