Na Karoli Vinsent
Katika kile ambacho
kinaonekana kama ni mbio za urais ndani ya chama cha mapinduzi CCM chama hicho
sasa kimeingia katika hofu juu ya waziri wa mambo ya nje BERNARD MEMBE katika
harakati zake wakizihusisha na mbio za kuusaka urais.
Mhe. Bernard K. Membe ambaye ni Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, ameonekana kuwa na nguvu ndani ya chama hicho kutokana na kitendo
chake kuendelea kufanya mikutano
mbalimbali ya kisiasa na isiyo ya kisiasa mikutano ambayo sasa imeanza
kuhusishwa na kampeni za kuusaka urais ndani ya chama hicho.
Mapema mwezi februari,mwaka huu Kamati
maalum ya maadili ya chama cha mapinduzi CCM ,ambayo iliwahoji vigogo sita wa
chama hicho tawala ambao walikuwa wanaonekana maeneo mbalimbali wakiendeleza
harakati za kumrithi Jakaya Kikwete ambae anatarajiwa kuondoka mwakani 2015.
Lakini kamati hiyo ya maadili ya chama
iliwafungia kwa mda wa mwaka mmoja makada sita wa chama hicho kutofanya
harakati zozote za kusaka urais ndani ya chama hicho makada hao ni Waziri
aliyejiuzulu Edward Lowassa,Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa
Berdanard Membe,waziri Mkuu wa awamu ya tatu Fredrick sumaye.
Mbali na hao wengine ni Waziri wa
ushirikiano wa Africa mashariki Samweli Sitta,Mbunge wa Sengerema Wiliam Ngeleja,waziri Stephen Wasira pamoja na
Naibu waziri wa mawasiliano,sayansi na Tekolojia January Makamba.
Licha ya Kamati ya chama hicho
kuwafungia makada hao kwa miezi 12,lakini Waziri Membe,ameonyesha kupuuza
maamuzi ya chama hicho kutokana na kufanya mikutano mbalimbali ambayo imekuwa
ikihusishwa bado na mbio za urais .
Membe amekuwa akipambana kwa hali na
mali kuhakikisha anakamata nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa Taifa hili.
Waziri Membe alianza kuonyesha kupuuza
kauli hiyo Wiki iliyopita alipokuwa anazindua Firamu ya Love Mwanza ambapo
alitumia nafasi hiyo kujitangaza Kisiasa,huku akitumia Kifua cha Rais Jakaya
Kikwete kupuuza Adhabu ya Kamati maadili ya chama cha mapinduzi,ambayo
walimzuia kufanya hivyo.
Membe alionekana kulitumia Jina la
Jakaya Kikwete kama njia ya kuwaogopesha Wasaka Urais wenzake ambao wamekuwa
wakiwakimya kwa sasa,ambapo alisema alichokifanya hapo kimetokana na kupewa
Baraka na Rais jakaya Kiwete ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM
aliyekuwa Juu wajumbe waliotua hukumu hiyo.
“Nilikutana na Rais Kikwete Juzi kumuaga
na kumueleza ujio wangu Jijini Mwanza kuwa nimeitwa na wasanii wa Filamu naye
alikubalia na kunitaka nifanya haraka na nisiache baada ya kurudi Jijini Dar
esSalaam nikampatie taarifa za kile nilichokishuhudia Jijini Mwanza,hivyo
nimekuja na Marafiki zangu ambao ni Frends of Membe”alisema Membe.
Achia mbali uzinduzi huo wa Filamu
mkoani mwanza,Waziri membe akafanya harakati zengine ambazo zinatafsiriwa kama
ni Harakati za kusaka urais baada ya kuandaa Semina ya Siku saba kwa Umoja wa
Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM, iliyofanyika ukumbi wa Msasani Club,Jijini
Dar es Salaam,ambapo katika semina ambayo iliandaliwa na Kufadhiliwa na Waziri
Membe.
Katika Semina hiyo ilivaa koti la nje
kwamba ilikuwa inawapa vijana wa CCM uwezo wa kuwajengea ili waweze kupambana
Na Umoja wa Katiba yaWananchi UKAWA,lakini mambo yalikuwa sivyo kutokana na
Semina hiyo ilionekana kama njia ya Waziri Membe kujinadi katika kusaka urais.
Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika
zinasema Waziri Membe alitoa zaidi ya Milioni 200,ili kugalimu Semina
hiyo,katika kufanikisha ambapo wajumbe walipata Posho pamoja na chukula,
Kufanya usaliti huu
kwa Waziri Membe,inatafsiliwa kama ni kuingia mpasuko ndani chama hicho
Kikongwe barani Afrika ambayo kipo madarakani,kutokana na Maamuzi waliyofikia
ya kuwafungia makada hao.
Akilizungumzia hili,Mjumbe wa
Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi CCM, kutoka mikoa ya kusini,ambaye
akutaka jina lake litajwe kwenye Mtandao huu,alisema ni wazi chama hicho
kinamwogopa Waziri Membe.
”Mimi mwenyewe nashangaa sana huyu waziri membe anavyoogopwa namna hii ndani ya
chama chetu,kwani ukweli huko wazi huyu anatumia ukaribu wake alikuwa nao kwa
Rais kikwete,ndio unamfanya kuzidisha kufanya harakati za kusaka urais,lakini
kwanini wasimpe adhabu kari huyu msaka urais”
“Kama wanaona wameshindwa kuwazuia ni
bora waache waendelee na harakati zao tu maana wengine tunawatu wetu tunataka
tuwasapoti tu na waruhusu tushindane tu”alisema mpashaji huyo wa Taarifa.
Kuonyesha huku jeuri kwa Waziri Membe,
kumekuja ikiwa Miezi miene kupita baada kamati ya Maadili ya chama hicho
kuwafungia makada hao.
Ambapo chama hicho kilifuata kanuni
ambapo ibara 6 (2) (1_5) ya maadili ya Viongozi wa Chama hicho inawazuia kutoa
mchango,misaada zawadi za aina yeyote,kukusanya michango na kufanya kampeni
bila ya kupata kibali kutoka kamati ya Siasa ya Halmashauri ya eneo husika.
No comments:
Post a Comment