Waziri
wa uchukuzi nchini Tanzania mh HARSON MWAKYEMBE amewafuza kazi katika uwanja wa
ndege muda huu watumishi takribani 13kutoka katika wizara za
kilimo,afya,pamoja na wizara ya mifugo na uvuvi,kwa kushindwa kufwata taratibu
za kazi katika uwanja wa ndege wa JK NYERERE jijini Dar es salaam.
Akizungumza
na Wanahabari muda huu ofisini kwake waziri MWAKYEMBE Amesema kuwa
watumishi wamekiuka sheria za kazi
kutokana na kuendekeza vitendo kama vya rushwa,ubaguzi uwanjani hapo jambo
ambalo Amesema kuwa hawezi kufumbia macho vitendo kama hivyo viendelee katika
uwanja huo
“Tunahangaika
sana kupambana na madawa ya kulevya katika uwanja wetu wa jk nyerere,sasa
wanajitokeza watu ambao sio waaminifu wanatuharibia sifa ya uwanja wetu kwa
sababu zao,kiukweli hatuwezi kuvumilia tabia hizo na kuanzia sasa saa sita
mchana sitaki kuwaona pale na nimeagiza waondolewe na polisi warudishwe
maofisini kwao”alisema MWAKYEMBE.
Hatua
hiyo imekuja baada ya kuwasilishwa kwa malalamiko kutoka nchi za uarabuni,india
na china kufanyiwa upekuzi tofauti na wengine na kuchukuliwa vyakula vyao na
bidhaa mbalimbali kinyume na sheria ambapo bidhaa hizo zimekuwa hazirudishwi
kwa wenyewe.
Waziri MWAKYEMBE amewataja wahusika hao kuwa ni -
Wizara
ya kilimo
1-TEDDY MWASENGE
2-ESTER KILONZO
3-REHEMA MRUTU
4-MARY KADOKAYOSI
5-KISAMO SAMJI
6-ANNETH KILIANGA
Wizara ya afya
1-AGNESS SHIRIMA
2-HAMIS BORA
3-VALERI CHUWA
4-ELINGERA MGHASE
5-REMEDIUS KAKULU
Wizara ya mifugo
na uvuvi
1-ESHI SAMSON NDOSI
2-ANNE SETEBE
Aidha waziri MWAKYEMBE ametoa onyo kali sana kwa
wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa JK NYERERE watakaoingia kwa sasa
kutojihusisha na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa sheria ikiwemo rushwa kwani
wizara yake haitawavumilia hata kidogo
No comments:
Post a Comment