Jeshi la kujenga taifa Tanzania JKT
leo limekanusha vikali taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa na watu mbalimbali
hususani mitandao ya kijamii kuwa kumekuwa na wanafunzi wanaofariki katika
mafunzo ya jeshi hilo katika makambi mbalimbali
Akizungumza na wanahabari muda huu jijini Dar es salaam
msemaji wa jeshi hilo ERICK KOMBA
Amesema kuwa kumekuwa na ujumbe mfupi umekuwa
ukitembea kwenye simu za mkononi pamoja na mitandao kuwa kuna idadi ya
wanafunzi ambao waliofariki katika
mafunzo ya jeshi hilo yanayoendelea katika makambi mbalimbali jambo ambalo Amesema
kuwa ni uwongo na taarifa hizo haziitaikii mema nchi ya Tanzania
KOMBA
amesemakuwa ukweli ni kwamba jeshi la kujenga taifa linasikitika kumpoteza kijana mmoja wa kike HONOTARA VALLLENTINE OISO
aliyefariki katika kikosi cha JKT OLJORO arusha kwa ugonjwa wa upungufu wa damu
uliosababishwa na malaria na sio vijana watatu kama ilivyoripotiwa kwenye
ujumbe unaosambaa.
Aidha Amesema kuwa wazazi wa kinana huyo wamekuri
kuwa mwanao alikuwa akisumbuliwa na tatizo hilo kwa muda mrefu.
Kwa sasa jeshi hilo lina vijana 38,634 wamaoendelea
na mamafunzo hayo ambapo amewataka vijana kuacha mara moja kujadili maswala ya
jeshi ndani ya mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment