Jaji
mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji MACK BOMANI Amesema
kuwa haoni hali yoyote ya kupatikana muafaka katika mgogoro iliojitokeza ndani
ya bunge la katiba kutokana na malumbano ya wabunge kuonekana ni makubwa sana
kiasi cha kutishia mchakato huo.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dare s salaam mapema leo
Amesema kuwa mgogoro ambao ulijitokeza bungeni juu ya muundo wa
serikali unaotakiwa ni jambo ambalo sasa limeanza kutishia muungano wetu.
“hili swala la muundo wa serikali ngapi
tuwe nazo tukicheza nalo litahatarisha muungano wetu kabisa”Amesema jaji BOMANI
Jaji
BOMANI Amesema kuwa sasa umefika wakati muafaka wa wabunge hao kuamua kuacha
kwanza swala la muundo wa serikali na kujadili mambo mengine ambayo yana
maslahi kwa taifa kutokana na kuonekana wazi kuwa mgogoro uliopo bungeni chanzo
chake ni kipengele cha muungano
“majadiliano
ya katiba mpya yasiishie tu kwenye idadi ya serikali kuna mambo mengi sana ya
kujadili,mi nashauri wa kwa wabunge wa bunge maalum,waliweke kando swala la
muundo wa serikali wajadili kwanza maswala mengine alafu hili swala la muungano
ni la kujadiliana na kuzungumza na mwishowe kukubaliana”Amesema bomani
Aidha jaji BOMANI amesema kuwa anakubaliana na
rasimu ya jaji warioba kwani ina mabo ambayo yana mustakabali wanchi yetu,hivyo
ni nafasi ya wabunge kutumia nafasi hii kutupa katia nzuri badala ya kuendeleza
malumbano kama ilivyojitokeza hapo awali.
Katika hatua nyingine jaji BOMANI amewashauri
wabunge wanaounda muungano wa UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI UKAWA warudi bungeni
kwani pamoja na kutokubaliana na mchakato huo lakini bado kuna mambo mengi sana
wanayotakiwa kuyajadili nje ya muundo wa serikali.
No comments:
Post a Comment