Na Karoli
Vinsent
UWEZEKANO wa
Mabiloni ya Fedha yaliyofichwa na Vigogo kwenye Mabenki mbalimbali nchini
Uswizi,sasa inazidi kuwa ni ndoto kwa
mafedha hayo kurudi kutokana na kutokuwa na nia ya Dhati ya Serikali ya Rais
Jakaya Kikwete kufanikisha Fedha hizo kurudi nchini,Mtandao huu umebaini.
Sakata la
Mabilioni hayo ya Uswisi yaliibuliwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto
Kabwe,ambaye naye kwa sasa ameoneka kama kufungwa mdomo kwenye sakata hilo la
kupambana ili fedha hizo ambazo ni chafu ili zirudi nchini.
Kwa mujibu
wa Vyanzo mbalimbali zinasema zaidi ya bilioni 200,zimefichwa na watanzania
kwenye Mabenki mbalimbali nchini uswisi,fedha hizo ambazo nyingi zimeonekana
kufichwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge,mawaziri wa awamu ya tatu nay a Nne,viongozi
wa juu wazamani wa Jeshi, pamoja na wasaka urais ndani CCM,
Uchunguzi
uliofanywa na Mwandishi wa Mtandao huu,umebaini hakuna nia ya Dhati iliyofanya
na serikali ya Rais kikwete kutokana kupuuza ushauri unaotelewa na watu
mbalimbali ambao waliweka mipango ya kuhakisha fedha hizo zinarudi ili zije
kuwanufaisha watanzania ambao wnaishi kwenye lindi la umasikini wa kutupwa
Upuuzi wa
kwanza uliofanywa na Serikali ya Rais Kikwete katika sakata hili ni pale ilipokataa
ushauri uliotolewa na Jaji mmoja kutoka Ufaransa ,Renaud Van Ruymbele kuhusu
hatua ambazo zinatakiwa kufaata ili kuwabaini watu walioficha pesa hizo kwenye
Akaunti mbalimbali za Mapenki huko
Uswisi.
Jaji huyo
ambaye anasifika katika Masuala hayo kutokana na Jinsi alivyoweza kuwabaini
Akaunt za wafaransi nchini Uswisi ambao walikwepa kulipa kodi.
Jaji huyo
Aliidokeza Serikali ya Tanzania kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Mahesabu ya
Serikali (PAC) Zitto Kabwe kwamba taarifa zote kuhusu Watanzania,Alishauri
kwanza Serikali ya Tanzania ipeleke Barua ya Maombi kwenye serikali ya Ufaransa
ikiwemo wizara ya Sheriaya Ufaransa.
Na endapo
Tanzania ikifanya hivyo Kikosi cha kazi kutoka wizara hiyo chini wa jaji huyo
wataanza kufuatilia pesa hizo zilizopo nchini uswisi
Lakini licha
ya Serikali ya Tanzania kupewa ushauri huo,lakini kile kinachonekana ni kupuuza
ushauri huo,ambao utapeleka pesa hizo kuwa ndoto kulejea kurudi nchini ni
kutokana na kitendo alichokifanya wiki iliyopita.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali nchini Fredilick Werema aliponukuliwa na Shirika la Habari la
Uingereza(Reuters) akisema kwamba serikali inafuatilia “Suala la urejeshwaji wa
Fedha hizo kupitia taasisi moja Binafsi inayoitwa ISCAR iliyopo Basel uswisi
ambayo inafanya kazi hiyo ya kurudisha fedha hizo kwa Garama Kamisheni kubwa
sana kwa serikali.
Uchunguzi
uliofanywa na Mwandishi wa mtandano huu umezidi kugundua ni ndoto fedha kuzidi
kurudi kutokana Taasisi hiyo ISCAR iliwai kulalamikiwa na serikali ya Nigeria
kwa kufanya kazi kusuasua ,ufuatiliwaji wa Mabilioni yalifichwa na kiongozi
Dikteta Sani Abacha.
Duru za
kisiasa zinasema ni ukweli usiopingika kwamba Serikali ya CCM,inazidi kufanya
maigizo kwa Watanzania kuhusu suala hili kwani imekosa nia ya Dhati ya
kufanikisha pesa hizi nyingi zirudi nchini kutokana na watu wengi walioficha
Fedha hizo huku Uswisi kuhusika katika maamuzi mbalimbali ya sheria hapa
nchini.
No comments:
Post a Comment