Na Karoli
Vinsent
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam
limefichua Siri ya kuongezeka Vitendo vya
ujambazi katika maBenki mbalimbali hapa nchini na kusema vitendo hivyo
vinasababishwa na Wamiliki wa Mabenki hayo kulipuuza Jeshi la polisi,
Kauli hiyo
ya Jeshi la polisi Kanda ya Dar es Salaam imekuja SIKU moja kupita baada ya watu wanaosadikiwa
kuwa ni Majambazi kuvamia katika Benki ya Stanbic tawi la Kariakoo liloko mtaa
wa Swahili na kukomba mamilioni ya pesa aliyokuwa nayo Mteja,
Kauli hiyo
imetolewa Mda huu na Kamishna wa Polisi kanda Maalum Dar Es Salaam,Suleiman
Kova wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari Jijini Dar Es Salaam,ambapo
alisema watu wanaochangia Vitendo hivyo vya Ujambazi kuzidi kuongezeka katika
Mabenki mbalimbali hapa nchini ni Wamiliki wa Mabenki kupuuza ushauri wa Jeshi
la Polisi ,
Uliowataka
waache kutumia walinzi wa Makampuni Binafsi peke yake,watumia na Walinzi kutoka
Jeshi la polisi.
“Nataka
niwambie waandishi hivi vitendo vya Uvamizi kwenye mabenki viemtokana na wamiliki wamabenki hayo kupuuza
ushauri wetu uliowataka kwenyes shuhuri za Ulinzi kwenye mabenki watumike
Polisi tu,lakini wao wakapuuza,ukitaka kuamini Nenda kwenye Mabenki
yanayolindwa na Polisi kama utaona kama kunauvamini wowote uonotokea,kwasababu
majambazi hao wanashindwa kuvamia kutokana na umakini wa Jeshi la Polisi”alisema
Kova
Kamishna
Kova,alisema kwa sasa la polisi limejipanga kuongea na Benki kuu(BOT) ambaye ni
kiongozi wa Benki zote hapa nchini na kutafuta ufumbuzi wa hili tatizo la
Mabenki Mengine kupuuza ushauri huo wa Jeshi la polisi.
Vilevile
jeshi hilo la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Limeeanza msako kali wa
kuwatafuta Majambazi watano waliovamia Jana kwenye Beki ya Stabic Tawi la
Kariakoo lilioko mtaa wa Shwahili majira ya mchana.
Kwa Mujibu
wa Kamishna Kova alisema watu wa tatu kati yao waliingia ndani ya Benki hiyo
wakiwa na Mifuko Mikubwa wakijifanya ni wateja wanapeleka Fedha nyingi katika
Benki hiyo,watu hao walipoingia ndani walianza kuwalazimisha kuvuka wigo wa
wateja wa kwaida na kutaka kuingia kwa nguvu kupora Fedha.
Ambapo Benki
hiyo ya Stabinc ina mitambo ya Aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na Vingora vya
Tahadhari,ikasaidia kwa majambazi hao kushindwa kuingia ndani kuiba pesa za
Benki hiyo kutokana na Vingora hivyo kupiga kelele na kuanza kuwapa uwoga
majambazi hao ,ambapo walifanikiwa kuiba pesa za mteja mmoja ambae alikuwa
anataka kuweka pesa kwenye benki hiyo,
Kova alisema
Majambazi hao walipotoka nje ya Benki hiyo walipiga Risasi Juu ili kuwapa Hofu
wananchi walikuwa Nje ya Benki hiyo,ambapo kwa Mujibu wa Kamishna Kova anasema
bado wanaendelea kuwafuatilia majambazi hao.
Katika Hatua
nyingine Jeshi hilo la polisi Limejipanga ipasavyo kwenye sikuku ya IDD El Haji
2014,ambapo jehi hilo limesema limepanga kushikirikiana na Vyombo mbalimbali
vya ulinzi na Usalama ikiwa ni pamoja na Kikosi
cha Zima Moto na Uokoaji,Kampuni Binafsi za ulinzi lengo ni kuhakikisha
wananchi wanafurahia kwa utulivu na amani kwenye sikuku hii.
No comments:
Post a Comment