Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa watu kumi wakiwemo watoto wawili,
wamefariki dunia papo hapo na wengine
saba wamejeruhiwa vibaya katika ajali
iliyohusisha magari mawili.
Ajali hiyo imehusisha gari ndogo ya abiria
maarufu daladala lenye namba za usajili T
237 BFB aina Toyota Hiace na gari kubwa
aina ya Fuso lenye namba za usajili T 158
CSV.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo
wamesema ajali hiyo imetokea maeneo ya Mbalizi baada ya Hiace iliyokuwa ikitokea
Mbeya mjini kuelekea Mbalizi kulivaa Fuso
lililokuwa likiingia barabarani.
Hata hivyo majina ya majeruhi na marehemu
hayajaweza kupatikana mara moja kutokana
na kuwa katika hali mbaya huku dereva
wa Fuso akitokomea baada ya tukio.
|
No comments:
Post a Comment