MWANASIASA,
wakili wa Mahakama Kuu, Mwanazuoni na mtetezi wa haki za Waislamu nchini, Prof.
Abdallah Safari, amejitosa katika kinyang'anyiro cha uchaguzi ndani ya Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Taarifa zilizothibitishwa na Prof. Safari mwenyewe zinasema, mwanasiasa huyo
mashuhuri nchini anatarajiwa kuchukua fomu wakati wowote kati ya leo na
kesho kuwania moja ya nafasi za juu za
uongozi. Ambapo Atawania umakamu mwenyekiti Tanzania Bara.
Akizungumza na Mtandao mmoja wa
Masuala ya kisiasa Nchini muda mfupi uliyopita, Prof. Safari amesema, ameamua
kugombea nafasi hiyo ili kutimiza adhima yake ya kuimarisha upinzani na
kuhakikisha chama tawala kinaondoka madarakani.
"Nilijiunga na Chadema nikitokea Chama cha Wananchi (CUF). Kule niligombea
nafasi ya uenyekiti. Kwa bahati mbaya sana, sikufanikiwa kushinda. Sasa
nimejiunga na Chadema na hivyo nataka kile ambacho ningekifanya CUF, nikifanye
Chadema," ameeleza.
Prof. Safari vilevile ambaye ni
mwandishi wa Vitabu mbalimbali nchini ikwemo Riwaya ya Nyoka mdimu na nyingine
alijiunga na Chadema miaka mitatu iliyopita, ambako mwenyekiti wake wa sasa,
Freeman Mbowe alimteuwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.
Tangu kujiunga na Chadema,
mwanasiasa huyo amekisaidia chama hicho katika maeneo mbalimbali, lakini kubwa
linalotajwa ni kuzima hoja za udini ambazo Chadema imekuwa ikipakaziwa na
wapinzani wake wa kisiasa.
Kuibuka kwa Profesa Safari kwenye
Kinyang’anyiro hicho kunazidi kuongeza idadi ya wagombea ndani ya chama hicho
katika nafasi za juu ambapo jana mwenyekiti wa chama hicho FREMAN MBOWE amechukua
fomu ya kutetea nafasi yake.
Mbowe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai,jana wakati
wa Mkutano na waandishi wa habari alithibitisha Rasmi kuchukua fomu ya kugombea
nafasi hiyo ya juu ya chama hicho ambacho ni kikuu cha upinzani nchini kwa sasa,\
Ambapo
Mbowe alianza kwa kueleza sababu
mbalimbali alizodai zimemshangaza kuona ni kwa nini awe yeye licha ya chama
kuwa na watu wengi wenye uzoefu na weledi.
Alisema kuwa ameshangazwa na namna makundi
mbalimbali yalivyojitokeza na kumtaka agombee ilhali wapenda majungu wanadai
amewapanga wakati hakuwa na mpango wa kugombea tena nafasi hiyo.
“Mimi sikuwaza kugombea na niliwahi kukataa
mara kadhaa. Nilikuwa nawaza kumpata ‘Mnyamwezi’ mwingine mwaminfu wa
kumkabidhi kijiti lakini Kamati Kuu iliyokaa hivi karibuni ilinikatalia kufanya
hivyo na mara kadhaa iliniomba nigombee tena,”alisema Mbowe.
Alisema hadi kufikia jana, alikuwa hajachukua
fomu na kwamba alipanga siku ya leo awe safarini kuelekea nchini Uingereza.
Mbowe alijigamba kuwa kutokuwa na uelewa na
weledi katika uongozi, kuliwafanya watu wengine kupotelea njiani kwa kutojua.
Alisema kuwa kuna wanaotumika na kuna
walioishiwa na nguvu na hata wengine kupata fedha kuhakikisha malengo ya
kuvuruga chama yanatimia lakini yeye alipambana hadi CHADEMA ikasonga mbele.
“Sikuwahi kuomba hata mara moja kugombea
nafasi hii katika vipindi vyangu vitatu. Mwaka 2004, niliombwa na aliyekuwa
Mwenyekiti Bob
Makani, nikakataa lakini jopo la Wazee liliniomba, nikakubali.
“Mwaka 2005, pia sikuomba kugombea urais, na
nafasi hiyo ilikuwa igombewe na Prof. Mwesiga Baregu ambaye mwishoni alijitoa
na nikaombwa nigombee mimi,”alisema.
Kwa mujibu wa Mbowe, mwaka 2009, aliombwa
tena kugombea uenyekiti na akalipiwa tena fedha za kuchukulia fomu na sasa
Wazee wa Kigoma wamekuwa wa kwanza kujitokeza na kumchukulia fomu.
“Hivyo, nakubali kugombea tena kuiongoza
CHADEMA kivingine, hakuna chama chochote kitakachokuwa na mtindo wa kufanya
hivyo hasa katika chaguzi zake mbalimbali,”alitamba Mbowe.
Aliongeza kuwa kwa sasa atafanya kazi kubwa
kivitendo zaidi na kutaka kila mwanachama kutoogopa na kutumika kwa kadri
atakavyoweza ili kuhakikisha wanakijenga chama.
Mbowe alikabidhiwa fomu hiyo na Mzee Mapindo
Saba kwa niaba ya wawakilishi wa Wazee wa mikoa ya Rukwa, Kigoma, Pwani, Dar es
Salaam, Manyara, Iringa, Njombe, Zanzibari
Mwenyekiti huyo ambaye amekuwa akifanyiwa
hujuma kutoka kwenye idara mbali mbali ikiwemo Idara ya Usalama ya Taifa,ambao walimfanyia hujuma
mwenyekiti huyo kwa Lengo la kudhohofisha Upinzani nchini.
No comments:
Post a Comment