Reuben De La Red kushoto amefunga mabao matatu peke yake Real ikishinda 3-1 Uwanja wa Taifa |
MSHAMBULIAJI Reuben de La Red amefunga mabao matatu peke yake, magwiji wa Real Madrid wakiiangusha Tanzania Eleven 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
De la Red alimfunga bao moja Mwameja Mohamed kipindi cha kwanza na kipindi cha pil akamtungua mara mbili Manyika Peter, wakati bao pekee la Stars, Real walijifunga wenyewe kupitia kwa Roberto Rojas.
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alimkabidhi mpira De La Red baada ya mechi kabla ya kuwakabidhi Kombe Real Madird kwa ushindi huo.
Katika mchezo huo, ambao wachezaji waliingia na kutoka, Real Madird walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, De La Red akimalizia pasi ya Luis Figo.
Luis Figo akimtoka Athumani China |
Mpira uliozaa bao hilo, ulianzia kwa kiungo Christian Karembeu, aliyezuia shambulizi la Tanzania na kuanzisha shambuizi zuri lililozaa matunda, akiuvuka msitu wa wachezaji wa wenyeji kwa umahiri mkubwa.
Tanzania Eleven ilisawazisha dakika ya 45 baada ya kona ya Mecky Mexime kuzua kizaa langoni mwa Real na Roberto Rojas akajifunga katika harakati za kuokoa baada ya Kali Ongala kuuparaza kwa kichwa.
.
|
Kipindi cha pili, De la Red alifunga bao kwa pili kwa penalti dakika ya 81 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Habib Kondo kwenye eneo la hatari.
Awali ya hapo, Figo alimtoka vizuri beki Mecky Mexime na kuingia hadi kwenye eneo la hatari akiwa kwenye nafasi ya kufunga akampasia De La Red ambaye alipiga nje.
De la Red alikamilisha hat trick yake dakika ya 88 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Tanzania Eeleven.
Wachezaji wa timu zote mbili wanatarajiwa kula chakula cha usiku na Mheshimiwa Rais Ikulu baadaye
No comments:
Post a Comment