KATIKA kuonyesha umakini waliokuwa nao katika kupambana na Matapeli, Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam,sasa linamshikilia na kumhoji mtu mmoja anayetambulika kwa jina la Robson Seif Mwakyusa Emmanuel (30) kwa tuhuma za kujifanya afisa wa polisi kikosi cha usalama barabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kamshina wa Polisi Kanda Maalum Suleiman Kova alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 2 mwaka huu huko Kata ya Chamazi ,Mbagala Majimatitu Wilaya ya Temeke akiwa amevalia sare za Polisi.
Alisema kuwa Mtuhumiwa huyo aliwahi kuwa askari wa Jeshi la Polisi aliyejiunga mwaka 2000 akiwa mwenye namba F2460 lakini alifukuzawa kazi kwa fedhea machi 3 mwaka 2014 huko kibaha Mkoani Pwani akiwa na cheo cha Stesheni Sajenti.
"Katika uchunguzi wetu wa awali unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akijitambulisha kuwa askari hivyo kufanikiwa kuwatapeli wananchi mbalimbali na kujipatia kiasi kikubwa cha fedha kwa njia za udanganyifu"alisema kova
Aliongeza kuwa katika gari hilo Polisi walipekua na kukuta Radio call 1 yenye namba GP380 aina ya Motorola,leseni za udereva 40,stakabadhi 2 za serikali zenye namba A0531562 na A1672464,police loss report mbalimbali,kofia,beji, na ratiba ya mabasi yaendayo mikoani pamoja na vitu vingine mali ya Jeshi la Polisi.
Aliendelea kusema kuwa mtuhumiwa huyo alipekuliwa hadi Nyumbani kwake ambapo alikutwa na pea 4 za sare ya Polisi ya kaki,pea 3 za sare za usalama barabarani,koti 1 la mvua la usalama barabarani,reflector 07 za kuongozea magari,kofia,mikanda ya jeshi,vyeo 3 vya Stesheni Sajenti.
Wakati huohuo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaama linawashikilia Majambazi wawili kwa tuhuma za kujihusisha na unyang'anyi wa kutumia silaa katika maeneo mbalimbali ya jijin la Dar es Salaam.
Kamishna Suleiman Kova alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa julai 30 mwaka huu huko Makumbusho Kijitonyama kufuatia msako mkali wa jeshi la Polisi.
"Watuhumiwa hao walipokaguliwa majumbani kwao walikamatwa na bastola 2 moja ni GROCK17 yenye namba B019259 iliyotengenezwa nchi ya Jamhuri ya CZECH ikiwa na risasi 13 ndani na magazine na nyingine ni bastola aina ya CHINESE iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi 1 ndani ya magazine"alisema Kova.
Kova aliwataja kwa majina watuhumiwa hao kuwa ni Fredy Steven (25) ambaye ni mfanyabiashara mkazi wa Kiwalani na Irene Nyange (36) mfanyabiashara mkazi wa Kijitonyama ambapo uchunguzi unakamilishwa na watuhumiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa
No comments:
Post a Comment