Na Karoli Visent
HUKU ikiwa bado wingu limetawala kuhusu hatima ya upatikanaji wa katiba Mpya,kutokana na upande umoja unaojiita Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia vikao vya Bunge Maalum la katiba na kusema hawatarudi kwa kile wananchokiita Mchakato huo umefanyiwa Hujuma na Chama cha Mapinduzi CCM.
Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu na Bunge, Willium Lukuvi amezidi kulichanganya Taifa baada ya kusema Vikao vya Bunge maalum Vitaendelea hata kama Upande mwengine wa UKAWA wasiporejea kwenye Bunge hilo
Kauli hiyo ameitoa leo Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo kauli hiyo ya Waziri Lukuvi inakuja huku kukiwa imebaki siku moja kabla ya Vikao vya Bunge Maalum la katiba Vitakavyoanza Kesho Mkoani Dodoma.
Waziri Lukuvi alisema kwa sasa wanakwenda Dodoma kujadili sura zilizobakia ambazo amesema zinawahusu watanzania zaidi kuliko sura zilizopita.
“Kwanza niseme kwamba Vikao vya Bunge maalum vitaendeleo kama kawaida na hapa mnaponiona mimi nikimaliza kuongea na nyinyi nakwenda moja kwa moja Mkoani Dodoma,na ikumbukwe tunakwenda kumalizia sura zilizobakia maana katika kipindi kile cha kwanza tulijadili sura mbili tu na sahivi tunakwenda kujadili sura zaidi ya tisa zilizobakia na tunakwenda bila uwoga kwamba kwanini UKAWA hawapo sisi hiyo sio tatizo”Alisema Lukuvi.
Waziri Lukuvi,ambaye ni Mbunge wa jimbo la Isimani CCM alizidi kusema wao hawashtushwi na kutokuwepo kwa UKAWA,kwani wajumbe waliobakia wanaweza kutunga katiba na haina haja ya kuwasubili watu wasiokuwa na tija juu ya upatikani wa katiba Mpya.
Katika hatua nyingine nao Wajumbe mbalimbali waliokuwepo kwenye iliyokuwa Tume ya katiba ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi,waliokuwa wakinzungumza kwenye mdahalo uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam ambao mdahalo huo ulirushwa moja kwa moja kwenye kitua cha ITV.
Ambapo walisema mchakato huo wa Katiba umehalibiwa na Rais Jakaya Kikwete kutokana na kuwadanganya wananchi kuhusu upatikani wa katiba mpya.
Kwa upande wake Mjumbe aliyekuwapo kwenye iliyokuwa tume ya Ukusanyaji wa Maoni Hawadh Ally alisema ameshindwa kuelewa elimu ya masuala ya uchumi aliyekuwano Rais Jakaya Kikwete kwa kitendo chake cha kusema muundo wa Serikali tatu ni mzigo.
No comments:
Post a Comment