Waziri wa viwanda na bisahara ABDALA KIGODA leo amezindiua rasmi maonyesho ya bidhaa za kichina nchini Tanzania maarufu kama BRANDS OF CHINA AFRICAN SHOWCASE 2014 maonyesho yanayoanza leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee na kumalizika tarehe 24 mwezi huu.
Akizungumza katika uzinduzi huo asubuhi ya leo waziri kigoda amewataka wafanya biashara wa china hapa nchini Tanzania kuhakikisha wanaleta bidhaa zilizo na ubora unaostahili katika soko la tanzania ili kuepuka madhara yanayotokana na uwepo wa bidhaa feki katika soko. Maonyesho hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka nchini tanzania yakiwa na lengo la kuonyesha bidhaa bora ambazo zinapatikana china. |
No comments:
Post a Comment