Mwenyekiti wa chama cha demcrasia na
maendeleo chadema na mbunge wa jimbo la hai mh FREMAN MBOWE leo
ametangaza rasmi kugombea tena nafasi a uenyekiti wa chama hicho kwa lengo la
kuendeleza harakati za chama hicho alizozianzisha.
Hatua hiyo imekuja baada ya wazee wa
baraza la wazee chadema na wazee kutoka kigoma kumwangukia na kumtaka
agombee tena huku wakimsifu kuwa amekisaidia sana chama hicho tangu akamate
uongozi hivyo ni vyema akaendelea kukiongoza tena chama hicho kwa lengo la
kutimiza malengo waliyojiwekea.
Akizungumza katika mkutano wa chama
hicho leo jijini dar es salaam MBOWE amesema kuwa amesikia maombi ya wazee hao
na yupo tayari kugombea tena nafasi hiyo ya uenyekiti wa chama hicho taifa.
huku akiwataka wanachama kuwa na imani na chama chao kwani mapambano bado
yanaendelea ya kuwakomboa watanzania.
Aidha MBOWE amesema kuwa wale ambao
wanajidanganya kuwa chama hicho kimepungua makali wakae mkao wa kula katika
chaguzi zijazo ndio watapata majibu ya mwaswali yao.
Baada ya kukubali ombi ilo wazee hao
walimkabidhi mwenyekiti huyo kiasi cha pesa shilingi elfu hamsini kwa ajili ya
kuchukua form ya kugombea tena nafasi hiyo ya juu katika chama hicho.
No comments:
Post a Comment