Kampuni
ya mawasiliano ya TIGO Tanzania kwa kushirikiana na shirika lisilo la
kiserikali nchini la REACH FOR CHANGE leo wamezindua shindano la wajasiriamali jamii liitwalo TIGO DIGITAL CHANGE MAKERS lenye
lengo la kuibua mawazo ua kibunifu ambayo yatasaidia kutatua matatizo
yanayowakabili watoto na vijana nchini.
Meneja mkuu wa tigo DIEGO GUTIEREZ leo amezindua
shindano hilo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo ametoa
wito kwa watu kishiriki ili wajiwekee katika nafasi ya kushinda fedha taslim
dola 20,000 ambazo kila mshindi atapewa azitumie katika utekelezaji wa mawazo
yao ya kibunifu.
Meneja huyo
alisema kuwa lengo lao ni kupata mawazo ya kibunifu ya kidigitali ambayo
yataleta na kutatua matatizo yanayo wakabili watoto kwa kiwango kikubwa huku
wakiendelea kuwekeza katika kukuza na kuimarisha huduma zao za mawasiliano
katika maeneo yote nchini.
Mawazo yatakayowakilishwa katika shindano hili
yanatakiwa kuonyesha uwezo wa kutumia simu kidigital teknologia ya habari na
mawasiliano kuleta ufanisi na utekelezaji wa mawazo husika,ambapo amesema kuwa
mtu anaweza kutuma mawazo yao kupitia www.tigo.co.tz/digitalchangemakers.
Kwa upande wake meneja wa nchi wa reach for change RICHARD
GORVERT amesema kuwa licha ya kupata kitita cha dola 20,000 washindi pia
watapewa vifaa vya kuendeleza utekezzaji wa mawazo yao ikiwa ni pamoja na
kuapata ushauri kutoka kwa wafanyakazi waandamizi kutoka tigo na reach for
change,aidha wataunganishwa na wajariamali wengine ambao tayari wamenufaika na
mpango huo.
meneja wa nchi wa reach for change RICHARD GORVERT akizungumza na wanahabari |
Mchakato huu wa kuwapata wajasiriamali jamii wa
kidigitali unaenda sambamba na na
mkakati wa TIGO wa kuendeleza maisha ya
kidigital nchini.huu ni mwaka wa tatu mfululizo ambapo kampuni ya tigo na reach
for change zimekuwa zikishirikiana kuwasaidia wajasiriamali jamii nchini ambapo
jumla ya wajasiriamali 6 wamenufaika na mpango huo katika kipindi hiki ambao
kwa pamoja na kupitia utekelezaji wa miradi yao wamewasaidia jumla ya watoto
zaidi ya 5700 nchini.
No comments:
Post a Comment